26.9 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Algeria kwazidi kuwaka moto

ALGIERS, ALGERIA

MAELFU ya wananchi nchini Algeria juzi waliingia mitaani kushiriki maandamano makubwa ya kupinga utawala wa Rais Abdelaziz Bouteflika, licha ya kiongozi huyo wa muda mrefu kutangaza kujiuzulu wadhifa wake mwanzoni mwa wiki hii, huku ikielezwa kuwa yalikuwa kipima joto kwa mamlaka nchini humo. 

Katikati ya wiki hii kumekuwa na mabadiliko na ishara mbalimbali za matumaini katika utawala nchini Algeria.

Mkuu wa majeshi, Ahmed Gaid Salah, alisema kuwa suluhisho la katiba linapaswa kupendekezwa kupatia ufumbuzi maandamano hayo, ambayo yanaendelea nchini Algeria.

Tayari wafanyabiashara, washirika wa karibu wa Rais Abdelaziz Bouteflika na wengi wao sasa wako chini ya uchunguzi wa awali kwa rushwa, hatua ambayo ni muhimu, kwa vile majina ya wafanyabiashara hawa pia yalikuwa yakitajwa katika maandamano. 

Miongoni mwa wafanyabiashara hao ni Ali Haddad, ambaye anatuhumiwa kuongoza katika rushwa kwa utawala wa Bouteflika yuko gerezani.

Baadhi wanaamini kwamba jeshi liko upande wa raia na kwamba lazima walishukuru na kulipongeza kwa kazi nzuri linalofanya. Wengine wanaamini kuwa kuheshimu Katiba ni kisingizio tu, wakati Katiba ilirekebishwa kwa zaidi ya miaka 20 iliyopita, na wana wasiwasi kuhusu jukumu la kijeshi katika utawala mpya.

Kwa upande wa waangalizi, wanasema ikiwa jeshi liliomba rais ajiuzulu, ni kutaka kulinda vema taasisi zilizopo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles