21.1 C
Dar es Salaam
Saturday, August 13, 2022

ALGERIA: CHAMA TAWALA CHAUNGA MKONO KUONDOLEWA MADARAKANI KWA RAIS ABDELAZIZ BOUTEFLIKA

Chama tawala nchini Algeria FLN kimeunga mkono kuondolewa madarakani kwa rais Abdelaziz Bouteflika, ambaye ametajwa kuwa mgonjwa na hivyo kutoweza kuongoza.

Uamuzi huo wa FLN umekuja siku moja baada ya Mkuu wa Jeshi nchini humo Luteni Ahmed Gaed Salah kusema kuwa uamuzi wa kikatiba unafaa kufanywa kumuondoa ofisini rais huyo.

Bouteflika ambaye yuko chini ya shinikizo kali baadaye alikubali kujiuzulu baada ya marekebisho ya kikatiba kupitishwa.

Mazungumzo yameanzishwa kujadili hatma ya siku za baadaye ya Algeria ambayo yataongozwa na mwanadiplomasia wa muda mrefu wa Umoja wa Mataifa Lakhdar Brahimi.

Maandamano yalianza mwezi mmoja uliopita wakati rais huyo mwenye umri wa miaka 82 aliposema kuwa anapanga kuwania urais kwa muhula mwengine .

Lakini watu waliendelea kuandamana hata baada ya kusema kuwa hatowania tena muhula mwengine na badala yake wakataka kufanyika kwa mabadiliko ya haraka.

Luteni jenerali Gaed Salah awali alinukuliwa akisema kuwa jeshi na raia wanafikiria kuhusu hatma ya taifa hilo akitoa ishara kwamba jeshi linaunga mkono maandamano hayo na kuongeza kuwa katiba ndio njia pekee ya kuleta uthabiti wa kisiasa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,592FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles