26.8 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 28, 2023

Contact us: [email protected]

Albamu ya Tiwa Savage yavunja rekodi MTN

TIWA-SAVAGELAGOSI, NIGERIA

MKALI wa muziki nchini Nigeria, Tiwa Savage, albamu yake imevunja rekodi ya kusikilizwa kupitia mtandao wa MTN Music nchini humo.

Albamu hiyo ambayo ameipa jina la Razz Enigma Dodobucci ‘R.E.D’ yenye nyimbo 16, imevunja rekodi ya kusikilizwa na idadi kubwa ya watu ndani ya saa 24 baada ya kuachiwa kwake.

Tiwa aliitayarisha albamu hiyo katika Studio ya Mavin Records ambapo wamewashirikisha baadhi ya wasanii kama vile Don Jazzy, Olamide, Dr. Sid, Iceberg Slim, 2Face, D Prince, Busy Signal na Reekado Banks.

“Ni furaha kubwa kuweza kuweka rekodi mpya kwenye mtandao wa MTN, ninaamini nyimbo zangu zinakubalika na ndio maana imeweka rekodi hiyo, kikubwa ni kujituma mwaka 2016 ili niweze kuweka rekodi nyingine,” alisema Tiwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
579,000SubscribersSubscribe

Latest Articles