29.2 C
Dar es Salaam
Sunday, September 19, 2021

Alalamikia upelelezi kesi uhujumu uchumi kuchukua miaka mitatu

NA KULWA MZEE-DAR ES SALAAM

MKURUGENZI wa Uthaminishaji Almasi na Vito Tanzania (Tansort), Archard Kalugendo, anayekabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi, amelalamikia upelelezi kutokamilika takribani mwaka wa tatu na ameomba Jamhuri wakamilishe haraka.

Kalugendo alifikisha ujumbe huo jana Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi wakati kesi hiyo ilipokuwa inatajwa.

Mbali na Kalugendo, mshtakiwa mwingine katika kesi hiyo ni mthamini almasi wa Serikali, Edward Rweyemamu  ambao kwa pamoja wanadaiwa kuisababishia Serikali hasara ya Sh bilioni 2.4.

Akiiwakilisha Jamhuri, Wakili wa Serikali, Nasua Candid alidai kesi hiyo imekuja kwa kutajwa na upelelezi bado haujakamilika, hivyo aliomba tarehe nyingine ya kutajwa.

Baada ya kudai hayo, mshtakiwa Kalugendo alidai wanakaribia miaka mitatu wakiwa gerezani na upelelezi haujakamilika, hivyo aliomba upande wa mashtaka kukamilisha ili kesi iweze kuendelea.

Hakimu Shaidi aliahirisha kesi hiyo hadi Mei 20 kwa kutajwa.

Kalugendo na Rweyemamu wanasota mahabusu kutokana na kesi hiyo kutokuwa na dhamana kisheria.

Kwa mujibu wa hati ya mashtaka, washtakiwa wanakabiliwa na mashtaka ya kuisababishia Serikali hasara ya Sh 2,486,397,982.54 wakidaiwa kutenda kosa hilo kati ya Agosti 25 na 31, 2017  katika maeneo mbalimbali ya mikoa ya Dar es Salaam na Shinyanga.

Washtakiwa wanadaiwa kwa pamoja na kwa vitendo vyao wakiwa wathaminishaji wa almasi wa Serikali na waajiriwa wa Wizara ya Madini, waliisababishia Serikali hasara ya Dola za Marekani 1,118,291.43  ambazo ni sawa na Sh 2,486,397,9.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
156,882FollowersFollow
518,000SubscribersSubscribe

Latest Articles