24.7 C
Dar es Salaam
Tuesday, October 8, 2024

Contact us: [email protected]

Al Shabab wafanya shambulio Kenya

NAIROBI, KENYA

Watu kadhaa wameripotiwa kujeruhiwa baada ya milipuko miwili mikubwa kutokea na ufyatuaji wa risasi katika Hoteli ya Dusit iliyopo eneo la Riverside jijini Nairobi.

Tukio hilo limetokea leo Jumanne Januari 15, ambapo kundi la kigaidi la Al Shabab limedai kuhusika na tukio hilo.

Jeshi la Polisi la Kenya limethibitisha kutokea kwa tukio hilo kupitia ukurasa wake wa Twitter na kuwatahadharisha watuamiaji wa barabara ya eneo hilo kutumia njia mbadala ili kuwarasishia polisi kufanya operesheni.

Polisi wakiongozwa na Mkuu wa Polisi wa Uchunguzi wa Jinai George Kinoti wamefika eneo hilo ili kuratibu operesheni ya uokozi wa watu waliokwama ndani.

Jumba hilo la kifahari lina hoteli kubwa na ofisi za watu mbalimbali.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles