22.7 C
Dar es Salaam
Saturday, August 13, 2022

Al Shabaab wadaiwa kuteka madaktari wa Cuba

NAIROBI, KENYA

MADAKTARIwawili raia wa Cuba ambao wanafanya kazi nchini Kenya wanadaiwa kutekwa nyara na watu wanaotajwa kuwa wapiganaji wa kundi la Al Shabaab katika mji wa Mandera, nchini humo.

Kwa mujibu wa taarifa ya Shirika la Utangazaji la Uingereza, BBC, tukio hilo limetokea mapema jana, wakati madaktari hao wakielekea kazini katika mji huo uliopo katika eneo la Kaskazini Mashariki mwa Kenya.

Aidha, limesema kuwa mwandishi wake katika eneo hilo la Mandera, Bashkas Jugosdaay, ameripoti kuwa walinzi wa madaktari hao wameuawa na watekaji ambao wamefanikiwa kutoroka kwa kutumia gari aina ya Probox. Hatima ya madaktari hao wa kigeni haijulikani hadi sasa.

Inaarifiwa madaktari hao wanaishi karibu na makazi ya gavana wa eneo hilo ambayo ni kilomita takriban 4 kutoka eneo la mpaka na Somalia. Haijulikani ni watekaji wangapi waliokuwa ndani ya gari hilo aina ya Probox, ambalo kwa mujibu wa mashuhuda lilikuwa limeegeshwa nje ya makazi hayo.

Milio ya risasi imesikika katika mji wa Mandera wakati maofisa wa usalama walipokuwa wanawasaka watekaji hao.

Akizungumza na waandishi wa habari, Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini Kenya, Charles Owino, amesema wahalifu hao walitoroka na gari hilo hadi mpakani na kuingia Somalia. Owino ameongeza kuwa, gari hilo la serikali ya Kaunti ya Mandera limepatikana na dereva wake anahojiwa.

Madaktari hao ni miongoni mwa wengine kundi la madaktari 100 kutoka Cuba waliowasili Kenya kwa ombi la serikali kuja kupunguza uhaba wa madaktari nchini humo.

Miongoni mwa madaktari walio kwenye kundi hilo kutoka Cuba ni wataalamu watano wa figo, wataalamu wa X-Ray, wataalamu wa mifupa na maungio na wataalamu wa mfumo wa neva. Madaktari hao wamekuwa wakitoa huduma na kushauriana na madaktari wengine katika maeneo tofauti nchini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,580FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles