24.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

Al Bashir alegeza msimamo kuhusu waandamanaji

KHARTOUM, SUDAN

RAIS wa Sudan, Omar al-Bashir amesema sheria kandamizi yenye utata na hali ngumu ya uchumi ndiyo vimechochea hasira miongoni mwa vijana wanaoongoza maandamano ya kumtaka aachie madaraka.

Matamshi hayo ya al Bashir anayekabiliwa na maandamano ya kila mara dhidi ya utawala wake, yameonyesha mabadiliko.

Awali, kiongozi huyo aliwafananisha waandamanji hao kuwa sawa na panya wanaopaswa kurejea kwenye mashimo yao.

Hivyo kauli ya sasa inatoa tafsiri kuwa ni sehemu ya mkakati mpya wa kusaka maridhiano na kupunguza ghadhabu za wanaompinga.

Akizungumza na wanahabari Ikulu mjini Khartoum, al-Bashir amekiri kwa mara ya kwanza kuwa sehemu kubwa ya waandamanaji ni vijana waliovunjwa moyo na hali ya uchumi ikiwamo mfumuko wa bei uliopandisha gharama za vyakula na ukosefu wa ajira.

Maandamano hayo yaliyoanza Desemba 19 mwaka jana yalichochewa na kupanda  bei za vyakula, ukosefu wa fedha za kutosha kwenye  benki na matatizo mengine ya  uchumi.

Hata hivyo, tangu hapo hasira zao zimeugeukia utawala wa miaka 30 wa Rais al-Bashir.

Polisi wamekuwa wakitumia gesi ya kutoa machozi na katika baadhi ya matukio risasi za moto kujaribu kuyasambaratisha maandamano hayo.

Pia, katika hali isiyotarajiwa, al-Bashir alikwenda mbali zaidi na kutoa ahadi ya kuwaachilia huru waandishi wa habari wanaoshikiliwa na utawala wake.

Bashir amesema waandishi wote wa habari ambao wamekamatwa na kufungwa kuhusiana na ghasia za maandamano wataachiwa huru. Inakisiwa idadi ya wanahabari walio jela kuwa 16.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles