AKOTHEE: SINA SURA LAKINI AKILI KICHWANI

0
628

NAIROBI, KENYA

MSANII ambaye anasumbua kwa sasa nchini Kenya, Estha Akothee ‘Akothee’ amesema, Mungu alimnyima sura, lakini amempa akili za kutosha.

Nyota huyo wa muziki mwenye watoto watano, amedai mbali na kufanya vizuri katika muziki, ameweza kutumia akili katika suala la uwekezaji ambao utamfanya azidi kujiongezea kipato kila siku.

“Mimi nilinyimwa sura lakini nikapewa akili hivyo ni heri nikaitumia ili nisije kuumia baadaye, utajiri nilionao ni kutokana na kujituma kwangu na kutumia akili vizuri.

“Ninaamini wapo ambao wamepewa sura nzuri lakini hawana lolote, wanashindwa kupambana na kutumia akili zao katika kuendesha maisha, hivyo sio lazima uwe na sura ndio uwe na fedha, kikubwa ni kutumia akili,” alisema Akothee.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here