AKOTHEE KUACHA MUZIKI KISA MPENZI WA KIZUNGU

0
791

 

 

NAIROBI, KENYA

MKALI wa muziki nchini Kenya, Esther Akothee ‘Akothee’, amesema kuna uwezekano akaachana na muziki baada ya kumpata mpenzi mpya ambaye ni ‘Mzungu’

Inadaiwa kwamba mpenzi huyo wa sasa hataki kusikia masuala ya muziki hivyo amemuomba mrembo huyo kuachana kabisa na muziki na achague kazi nyingine ya kufanya.

Hata hivyo, mapema mwaka huu msanii huyo mwenye watoto watano, aliwahi kusema kuwa katika maisha yake hawezi kusumbuliwa na mwanamume yeyote kwa kuwa anaweza kuendesha maisha yake mwenyewe.

“Mzungu wangu yuko moyoni, lakini amenishangaza kuniambia niachane na muziki, hivi inawezekana kweli? Sidhani kama ninaweza kufanya hivyo lakini ninampenda sana na muziki ni sehemu ya maisha yangu hadi nafikia hatua hii,” alisema Akothee.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here