31.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

AKIBA YA SUKARI NCHINI INATOSHELEZA MIEZI MITATU

 

 


Na ESTHER MBUSSI-DODOMA

Serikali  imesema sukari iliyopo nchini kwasasa, inatosheleza mahitaji ya miezi mitatu.

Wakati huohuo, bei ya juu ya suka imetajwa kuwa ni Sh 2,900 ambayo ndiyo inayouzwa Mkoa wa Kigoma, huku Kagera ikiuzwa chini ya Sh 2,400.

Akiwasilisha bungeni taarifa ya hali ya sukari nchini, Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage, alisema kwa mwezi wenye unafuu Kigoma sukari huuzwa Sh 2,850 na Morogoro Sh 2,400.

Alisema mahitaji ya sukari nchini yanakadiriwa kuwa tani 670,000 ambapo tani 515,000 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na tani 155,000 kwa matumizi ya viwandani.

“Uzalishaji wa sukari kwa viwanda vyetu vitano vya ndani kwa 2018/19, unakadiriwa kuwa tani 353,651 kwa ajili ya matumizi ya kawaida na hakuna kiwanda kinachozalisha sukari kwa ajili ya matumizi wa viwandani.

Hivyo basi nakisi ya sukari nchini ni takribani tani 316,349 ikihusisha tani 161,349 kwa maana ya matumizi ya kawaida na tani 155,000 kwa ajili ya matumizi ya viwandani ambazo zitabidi kuagizwa kutoka nje ya nchi.

“Viwanda vyote vitano vya Kilombero, Manyara, Kagera, Mtibwa na TPC vilivyopo nchini vinaendelea na uzalishaji, mbapo hadi kufikia Septemba 5, mwaka huu tani 119,671.19 ambayo ni sawa na asilimia 33.82 ya malengo ya uzalishaji kwa viwanda vyote vitano, zilikuwa zimezalishw ,” alisema.

Alisema tathmini ya tasnia ya sukari kwa kipindi cha miezi sita kuanzia Machi hadi agosti mwaka huu, inaonyesha kuwa bidhaa hiyo inapatikana bila matatizo katika maeneo yote nchini.

Mwijage alisema Serikali imewaagiza wenye viwanda kuboresha mfumo wa usambazaji sukari nchini kwa lengo la makusudi la kupunguza makali ya bei ya sukari kwenye mikoa hiyo ukilinganisha na mikoa mingine.

“Utafiti uliofanywa na Kampuni ya LMC International ya Uingereza mwaka 2014 kuhusu gharama ya kuzalisha tani moja ya sukari katika tasnia ya sukari nchini ulibaini kuwa inagharimu wastani wa Dola za Marekani 705, kwa kutumia kiwango cha kubadilishia Dola kwa shilingi kwa sasa, hii ni sawa na Sh 1,607 kwa kilo moja.

“Utaona hapa kuwa bei ya sukari inategemea kuimarika kwa Dola ya Marekani dhidi ya Shilingi ya Tanzania  hii ni kwa sababu viwanda vya sukari vinatumia mafuta, mitambo na vipuri.

“Bidhaa ambazo bei zake hupanda pindi Dola ya Marekani inapoimarika dhidi ya shilingi. Hii moja ya sababu inayochangia bei ya sukari kuwa kubwa au kubadilika mara kwa mara na sababu nyingine ni mashamba mengi ya miwa kulimwa kwa kutumia mtindo wa zamani ambao hauna tija kubwa,” alisema.

Alisema kutokana na matokeo ya tathmini hiyo, serikali itaendelea kuhakikisha wananchi wanapata sukari wakati wote na kwa bei stahiki, ambapo pia serikali imetoa maelekezo kwa kwa viwanda vyote kuwasilisha mapendekezo mapya juu ya mfumo wa kusambaza sukari nchini.

“Ushauri wa kusambaza sukari nchini ili kusaidia kushusha bei, wazo hilo haliwezi kuleta matokeo chanya hii ni kutokana na ukweli kwamba mikioa yote nchini hivi sasa ina sukari ya kutosha lakini pia bei ya sukari inategemea gharama za uzalishaji, kodi na gharama ya usafirishaji vigezo ambavyo si rahisi kuviepuka.

“Aidha, wawekezaji wapya wanaoanza kuwekeza katika uzalishaji wa sukari nchini wanapewa maelekezo ya ulimaji na utunzaji miwa kwa njia zinazoongeza tija kubwa kwa lengo la kupunguza gharama ya uzalishaji na hatimaye kumpatia mlaji wa mwisho bei nafuu,” alisema Mwijage.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles