AKAMATWA NA NYARA ZA SERIKALI

0
1185

Na Beatrice Mosses                       |                             


Jeshi la polisi mkoani Manyara limemkamata mtu mmoja, Bura Mayomba (55), mkazi wa kijiji cha Ngoley Kata ya Mwada wilaya Babati akiwa na nyara za serikali ambayo ni mayai ya mbuni.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Manyara leo Septemba 5, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, Augustino Senga amesema mtuhumiwa huyo alikamtwa Septemba 3, mwaka huu akiwa na mayai tisa ya mbuni.

“Ofisa Wanyama Pori Wilaya ya Babati, Jackson Robert, akiwa na askari wa Burunge kwa kushirikiana na askari polisi, walifanya doria ya muungano, ambapo walimkamata mtuhumiwa nyumbani kwake akiwa na mayai tisa ya Mbuni akiwa ameyaficha katika dumu lenye ujazo wa lita 20 nyuma ya nyumba yake.

“Kukamatwa kwa mtuhumiwa na mayai haya tisa ya Mbuni ambayo ni nyara za serikali na kujimilikisha bila kibali ni idhini ya serikali au Mkurugenzi wa Wanyama Pori Tanzania,” amesema.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here