31.2 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Akamatwa baada ya kumpigia simu waziri akidai ana corona

 DAMIAN MASYENENE – SHINYANGA 

JESHI la polisi mkoani Shinyanga, linamshikilia Mussa Kisinza (25) mkazi wa Kijiji cha Mwakitolyo,Shinyanga vijijini kwa madai ya kutoa taarifa za uongo baada ya kumpigia simu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, na kudai ana virusi vya Corona 

Hatua hiyo imekuja ikiwa ni siku chache toka jeshi hilo mkoani Shinyanga kusema limemkamata Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Mariam Sanane (23) kwa tuhuma za kuchapiaha takwimu za uongo kuhusu virusi vya corona kwenye mtandao wa kijamii wa WhatsApp. 

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, ACP Debora Magiligimba, alisema mtuhumiwa huyo ambaye ni mkulima, baada ya kutoa taarifa hizo kwa waziri timu ya madaktari inayotoa huduma kwa washukiwa wa corona katika Wilaya ya Shinyanga vijijini, ilifika kijijini hapo kutoa huduma kwa mtu huyo (Mussa Kisinza) lakini akazima simu yake. 

“Timu ya wataalamu ilifika Kijiji cha Mwakitolyo Namba 2 kutoa huduma kwa mhusika lakini alizima simu yake na kusababisha timu ya madaktari kushindwa kumpata hivyo kusababisha taharuki. “ Aprili 15, mwaka huu saa 1:00 asubuhi kikosi kazi cha askari wa makosa ya kimtandao walifika eneo la Mwakitolyo Namba 2 na kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa akiwa anaendelea na shughuli zake za machimbo na kumfikisha zahanati ya kijiji hicho ambapo timu ya madaktari ilimfanyia vipimo vya awali vya magonjwa nyemelezi yanayoashiria kuwepo kwa uwezekano wa mtu kuwa na COVID -19,” alisema Kamanda Debora. 

ACP Debora alieleza baada ya timu ya wataalam kumfanyia vipimo mtuhumiwa huyo, majibu yalionyesha hakuwa na dalili za magonjwa hayo na baada ya kuhojiwa akakiri kutoa taarifa hiyo na kwamba baadae aliamua kuiharibu laini yake ya simu kwa kuivunja. 

Kamanda huyo ametoa wito kwa wananchi kuacha masihara juu ya virusi vya na mtu yeyote atakayetoa taarifa za uongo juu ya maradhi hayo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake. 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles