26.1 C
Dar es Salaam
Friday, December 9, 2022

Contact us: [email protected]

Ajiua kisa mke amemaliza fedha kununua runinga

HASSAN DAUDI NA MITANDAO

HIYO imetokea huko Bengaluru, India, ambapo mwanamume aliyetajwa kwa jina la Srinad amejinyonga na kilichowashangaza wengi ni kilichomsukuma kufikia uamuzi huo.

Srinad (39), alijiua mwishoni mwa wiki iliyopita baada ya kukerwa na hatua ya mkewe kumaliza kiasi cha fedha alichokuwa amekopa ofisini.

Kwa mujibu wa taarifa, jamaa alikuwa amechukua mkopo katika kampuni anayofanya kazi kwa lengo la kununua vitu vya ndani, ikiwamo televisheni ya kisasa ‘flati’.

Hata hivyo, siku aliyorudi na kukuta mkewe aitwaye Rekha ameitumia fedha yote kwa matanuzi yasiyo na msingi, ndipo mwanamume huyo alipoona ajiue, kwa mujibu wa taarifa ya polisi.

Polisi wameweka wazi kuwa wataendelea kumshikilia Rekha kwa uchunguzi zaidi juu ya tukio hilo.

Kwa upande mwingine, polisi taarifa ya polisi imemtaja Rekha kuwa  ni mwanamke aliyekuwa akimtesa mkewe kwa kipindi kirefu cha ndoa yao.

Mateso hayo ni pamoja na kumalizimisha jamaa aandike jina la baba yake, kwa maana ya baba mkwe, kwenye nyaraka za umiliki wa baadhi ya mali zake.

Tukio kama hilo liliwahi kutokea mjini Sichuan, China, lakini haikufikia hatua ya mwanamume kujiua, japo alikuwa kwenye harakati hizo.

Jamaa huyo mwenye umri wa miaka 29, alikerwa na kitendo cha mkewe, Zhan, kumaliza Dola za Marekani 58,000 (zaidi ya Sh mil. 130) katika matumizi ya ajabu tu.

Bibiye huyo alitumia kiasi hicho kununua mabegi ya mkononi, manukato na vipodozi kupitia biashara ya mitandaoni.

Mara baada ya kugundua kuwa mkewe amefanya upuuzi huo, jamaa anayeitwa Wang alitaka kujirusha kutoka ghorofani na ndipo majirani walipopiga simu polisi kuomba msaada.

Polisi walipofika eneo la tukio, walilazimika kumuomba Wang aachane na uamuzi wake wa kutaka kujiachia kutoka ghorofa ya 33 lakini alionekana mwenye hasira mno.

Ilichukua muda mrefu lakini hatimaye walifanikiwa kumshawishi na kuingia naye ndani kwa mazungumzo.

Wang akikiri kuwa kwenye kipindi kigumu kutokana na msongo wa mawazo, akisema mshahara wake ni mdogo lakini mkewe hajaonesha kujali, badala yake anatekekeza fedha kwa matumizi ‘yasiyo na kichwa wala miguu’.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
205,735FollowersFollow
558,000SubscribersSubscribe

Latest Articles