22.1 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 31, 2023

Contact us: [email protected]

AJIRA HATARISHI ZENYE MSHAHARA MNONO NCHINI UINGEREZA

Na Joseph Lino

Watu wengi hudhani kuwa kusoma ni miongoni mwa mambo ambayo yanaweza kukuepusha na ajira hatarishi, jambo ambalo si kweli.

Nchini Uingereza kuna taaluma ambazo huonekana hatarishi licha ya watu kuzisomea na baadaye kuajiriwa.

Ripoti ya Health Service Excutive (HSE), nchini Uingereza iliyotolewa hivi majuzi, ilionesha kuwa kuna baadhi ya taaluma ambazo husababisha vifo vingi kwa wafanyakazi pindi wanapokuwa kazini.

Ripoti hiyo iliangalia idadi ya vifo vya wanataaluma kutoka kwenye sekta kadhaa kuanzia mwaka 2010 hadi 2016.

 

Taaluma ya kilimo

Ajira za kilimo nchini Uingereza ni moja ya taaluma hatarishi zaidi  kutokana na vifo vya wanataaluma 167 vilivyotokea kati ya mwaka 2010 hadi 2016.

Hii ni kutokana na kutumia mashine nzito na mazingira ya kazi kama kuwa karibu na wanyama wakiwamo ng’ombe wa maziwa wenye uzito wastani wa kilo 680. Hii inamanisha kuwa mazingira yaliyopo mashambani ni hatari kwa afya.

Licha ya kuhatarisha maisha ya wafanyakazi, mshahara wa mkulima wa kawaida ni wastani wa Sh milioni 64.6 sawa Paundi za Uingereza 22,157 kwa mwaka.

Ujenzi

Takriban nusu ya vifo vinavyotokea katika sekta ya ujenzi nchini Uingereza, husababishwa na kuanguka kutoka umbali mrefu wakati ujenzi ukiendelea, pia vitu vinavyodondoka kutoka juu vinakuwa hatari kwa mafundi ujenzi. Vifo 101 vimeripotiwa kutokea  mwaka 2010/16. Wastani wa mshahara kwa mafundi ujenzi nchini humo ni Sh milioni 52.7 (£18,080) kwa mwaka.

Udereva wa malori makubwa

Ajira ya kuendesha malori ya kubeba mizigo ni miongoni mwa kazi hatari nchini humo. Madereva wengi hufariki katika ajali pindi wanaposhindwa kudhibiti malori hayo. Hata hivyo, robo ya vifo vya madereva hao husababishwa na magari mengine barabarani. Madereva 41 wamepoteza maisha nchini Uingereza katika ajali barabarani. Mshahara wa dereva wa lori nchini Uingereza ni Sh milioni 68.2 (£23376) kwa mwaka.

Wapaka rangi

Taaluma ya kupaka rangi  hauwezi kudhani kama ni hatari, lakini nchini Uingereza wapaka rangi wengi wanafanya kazi katika majengo marefu hivyo kujikuta wakihatarisha maisha yao. Vifo 18 kati ya 28 vinatokana na kuanguka kutoka juu ghorofani pindi wanapopaka rangi.

Mpaka rangi nchini humo hulipwa wastani wa Sh milioni 69.3 (£23,796) kwa mwaka.

Fundi magari

Mafundi magari hutumia muda mwingi katika kufanya kazi chini ya magari makubwa. Hali hiyo huwafanya wakati mwingine wajikute wakipata ajali mbaya katika mazingira ya kazi. Mshahara wa fundi wa aina hiyo kwa mwaka ni wastani wa Sh milioni 82.7 (£28,369).

Fundi umeme na mabomba

Wengi hufikiria kuwa changamoto kubwa ya mafundi umeme kwenye kazi yao ni kupingwa shoti (electrocution), lakini ajali au vifo vya mafundi umeme ni kuaguka kutoka juu. Mshahara wao kwa mwaka ni wastani wa Sh milioni 87.4 (£30,042) wakati mafundi bomba hulipwa wasatani wa Sh milioni 99.6 (£34,228).

Uhandisi

Uhindisi ni miongoni mwa taalumu zenye mazingira hatarishi nchini Uingereza. Mara nyingi wahandisi huangukiwa na vifusi, kugongwa na magari, kupingwa na shoti ya umeme na hata joto kali huweza kuwasababisha kufariki dunia. Mshahara wa mhandishi unafikia Sh milioni 114.2 (£39,186) kwa mwaka.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,205FollowersFollow
567,000SubscribersSubscribe

Latest Articles