23.3 C
Dar es Salaam
Sunday, October 6, 2024

Contact us: [email protected]

Ajifungua bila kujua ana ujauzito wala kuhisi uchungu

Mwandishi Wetu

EBONY Stevenson (18), alijikuta akiwa amejifungua mtoto wa kike baada ya kuzirai kwa muda wa siku nne kutokana na maumivu ya kichwa yaliyokuwa yakimkabili.

Baada ya kupata fahamu alishangaa kukuta amejifungua mtoto wa kike.

Msichana huyo kutoka Oldham nchini Uingereza, hakuwa akifahamu kama ana ujauzito, alikuwa hajihisi vizuri akaamua kwenda kupumzika lakini baada ya hapo hakufahamu nini kinaendelea.

Ebony alikutwa akiwa amelala kwa muda mrefu hivyo mama yake akapata hofu na kuamua kumpeleka hospitali kupata tiba, ambako alibainika kuwa na ujauzito.

Mtoto wake alikuwa amejificha katika mfuko wa uzazi ambao pia ulikuwa umejificha, jambo ambalo huwa linatokea mara chache.

Kati ya miji miwili ya uzazi, mmoja ulikuwa unaendelea kumfanya dada huyo apate hedhi huku mji mwingine ukiendelea kukuza mtoto.

Mji huo wa mimba ulikuwa umekaa mgongoni jambo ambalo lilisababisha ujauzito usionekane.

Msichana huyo ambaye ni mwanafunzi wa michezo na yoga hakuwa na mwonekano kwamba ni mjamzito, hakuwahi kuugua muda wa asubuhi wala kukosa hedhi.

Ebony ambaye amejifungua kwa mara ya kwanza, anasema anashangazwa na kile kilichomtokea, kupata mtoto bila kufahamu kwamba ni mjamzito ni muujiza kwake.

“Nina hofu namna nitakavyoweza kumlea mtoto wangu, maana sikumuona hata wakati anatoka tumboni kwangu au kuhisi kuwa alikuwa tumboni kwangu, ila nafikiri ni mtoto mzuri,” anasema Ebony.

Ebony alifanyiwa upasuaji wa dharura ili ajifungue, saa tatu baada ya kushtuka kwa nguvu kutoka kwenye usingizi mzito.

Mama yake binti huyo Stevenson, mwenye umri wa miaka 39 anasema alipiga simu ya dharura baada ya mtoto wake kuanza kuumwa na kuanguka bafuni.

Imeandikwa kwa msaada wa BBC

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles