23.1 C
Dar es Salaam
Monday, September 25, 2023

Contact us: [email protected]

Ajibu awasihi Yanga kuwa watulivu

Na MWANDISHI WETU

– DAR ES ALAAM

NAHODHA wa timu ya Yanga, Ibarahim Ajib, amewataka mashabiki wa klabu hiyo kuwa watulivu na wasikate tamaa katika michezo ya Ligi Kuu Tanzania Bara iliyosalia.

Akizungumza mara baada ya timu ya Yanga kufungwa na Lipuli ya Iringa katika mchezo wa nusu fainali ya FA uliofanyika juzi kwenye Uwanja wa Samora mjini Iringa, Ajib alisema kuwa katika mchezo wa soka kuna matokeo matatu.

Alisema kuwa timu inaweza fungwa, kutoka sare ya kushinda, hivyo mashabiki wanatakiwa kuyazingatia hayo. Alisema kuwa timu ya Lipuli si mbaya na kufungwa kwao ni bahati mbaya, kwani walipambana katika dakika zote 90.

“Naomba mashabiki wetu wawe watulivu katika kipindi hiki, tumepoteza  mchezo wa  nusu fainali dhidi ya Lipuli, lakini tutahakikisha tunashinda michezo ya Ligi Kuu iliyosalia, tukiomba wapinzani wetu Simba wateleze ili tuweze kuwa mabingwa,” alisema.

Alisema kuwa, anafahamu kuwa mashabiki wanaumia pale timu yao inapokosa nafasi ya kushiriki mashindano ya kimataifa, lakini hilo lisiwavunje moyo, watapambana hadi mwisho wa safari. Yanga inatarajia kucheza na Biashara kesho  katika mfululizo wa Ligi Kuu ya soka Tanzania Bara.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,718FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles