25.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 1, 2021

Ajib apewa ujanja Simba

Theresia Gasper-Dar es Salaam

KOCHA wa viungo wa Simba, Adel Zrane, amemshauri  kiungo mshambuliaji, Ibrahim Ajib  kutumia muda huu kujiweka fiti zaidi ili watakaporudi aweze kupata nafasi ya kucheza mara kwa mara.

Kauli hiyo ya Zrane imekuja baada Serikali kusimamisha Ligi Kuu Tanzania Bara kwa siku 30 ili kupunguza kasi ya maambukizi ya ugonjwa wa Corona, ambao umeanza kushika kasi nchini.

Ajib ameshindwa kupenya kwenye kikosi  cha Wekundu wa Msimbazi, licha ya kusajiliwa kwa mbwembwe nyingi akitokea Yanga msimu uliopita alipokuwa mchezaji wa kutumainiwa.

Kiwango cha nyota huyo kipenzi cha mashabiki wa Simba kimeonekana kushuka tofauti na msimu uliopita ambapo alimaliza akiwa na mabao 10 na kupiga pasi za mwisho ‘assist’ 15.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Zrane alisema mchezaji huyo anatakiwa kuwa makini zaidi, huku akimtaka kutumia muda huu wa mapumziko kufanya mazoezi binafsi ili kujiweka fiti zaidi.

Alisema endapo atazingatia ushauri na programu aliyompa, anaamini Ajib atarudi kikosini na kupata mwingi wa kucheza.

 “Katika siku za hivi karibuni kiwango cha Ajib kimeonekana kushuka, hivyo anatakiwa kufanya mazoezi ya nguvu na kuwa makini zaidi hasa katika muda wa mapumziko,” alisema.

Zrane alisema kila mchezaji amemwangalia na kumpa programu maalum itakayomsaidia katika kipindi hiki cha mwezi mmoja.

“Baada ya mapumziko ya mwezi mmoja tumewapa wachezaji maelekezo ya kufanya kwani nimemwangalia kila mmoja na kumpangia kitu gani afanye kwani wote hawapo sawa ikiwa pamoja na gym,” alisema.

Alisema mbali na hayo pia amewapangia jinsiya kula mlo kamili kwa mchezaji ambao utaweza ukawaweka kuwa fiti.

Kocha huyo alisema anataka kwa sasa kuna baadhi ya wachezaji ambao wanatakiwa kujikinga zaidi na kuangalia afya zao katika kipindi hiki kutokana na kazi zao.

Simba inashika usukani katika msimamo wa ligi ikiwa na pointi 71 kati ya mechi 28 walizocheza wakishinda michezo 23 sare mbili na kupoteza mara tatu.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,530FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles