28.7 C
Dar es Salaam
Wednesday, January 19, 2022

Ajax wamtaka anayesota benchi Spurs

AMSTERDAM, Hispania

KLABU ya Ajax inaangalia uwezekano wa kumsajili kiungo wa pembeni wa Tottenham, Steven Bergwijn.

Mholanzi huyo anapitia kipindi kigumu tangu Antonio Conte awe kocha, ambapo amecheza dakika 13 tu, huku akiwa hajaanza hata mara moja.

Bergwijn (24), hayuko peke yake kwenye majanga hayo kwani hata Dele Alli, Tanguy Ndombele na Joe Rodon nao wamekalia kuti chini ya kocha huyo raia wa Italia.

Katika ofa yao, Ajax wameitaka Tottenham iwaruhusu wamchukue kwa mkopo Mholanzi mwenzao huyo kupitia usajili wa dirisha dogo, Januari, mwaka huu.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
175,312FollowersFollow
531,000SubscribersSubscribe

Latest Articles