30.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Ajali za majini zazidi kutikisa DRC

KINSHASA, DRC

USAFIRI wa majini umeendelea kuwa jinamizi kwa wasafiri nchini hapa, baada ya ajali ya boti kugharimu maisha ya watu 30 huku wengine zaidi ya 300 wakiwa hawajulikani waliko.

Kwa mujibu wa Shirika la Utangazaji la Uingereza – BBC, ajali hiyo ambayo ni mwendelezo wa majanga ya majini nchini hapa, ilitokea juzi usiku katika Ziwa Mai-Ndombe, lililopo eneo la Inongo Magharibi na hadi sasa bado mamia ya waliokuwa wakisafiri na boti hiyo hawajapatikana.

“Hadi sasa tumeshapata maiti 30, wanawake 12, watoto 11 na wanaume saba.

“Idadi hiyo ya vifo ni ya muda huu, na yaweza kubadilika muda wowote,” Meya wa mji wa Inongo, Simon Wemba aliliambia Shirika la Jabari la Ufaransa – AFP.

Wemba aliongeza kuwa ni vigumu kujua kwa hakika boti hiyo ilikuwa imebeba abiria wangapi na yawezekana ilikuwa imesheheni wahamiaji haramu.

Alisema kuwa waliookolewa katika ajali hiyo ni watu 183 na chanzo kinatajwa kuwa ni hali mbaya ya hewa.

Boti hiyo pia inaaminika kuwa ilipakiza idadi kubwa ya walimu ambao walikuwa wanaelekea kupokea mishahara yao.

 Ajali hiyo imetokea ikiwa ni mwezi mmoja  tangu watu 167 walipofariki dunia katika ajali mbili za majini nchini hapa na kumlazimu Rais Felix Tshisekedi kuamrisha kuwa abiria wote wa vyombo vya majini wavalishwe maboya muda wote wa safari.

DRC ambayo ndiyo nchi kubwa zaidi barani Afrika, inategemea mito na maziwa kama njia za usafiri wa watu na mizigo na kuunganisha maeneo kadhaa ya nchi ambayo ni vigumu kufikika kupitia barabara.

Hata hivyo, usafiri huo umekuwa wa hatari kwa usalama, na licha ya Serikali kuchukua hatua mbadala kutafuta ufumbuzi katika suala hilo bado hali si shwari.

Ajali nyingi husababishwa na matatizo ya kiufundi ya vyombo vya majini pamoja na kujaza watu kupita kipimo.

Idadi ya vifo huwa kubwa sababu abiria hawavai maboya ya uokozi, lakini pia raia wengi wa nchi hii hawajui kuogelea.

Septemba mwaka jana, watu 27 walipoteza maisha baada ya boti yao kuzama na wengine 26 wakapoteza maisha Julai mwaka huo ikiwa ni baada ya wengine 90 kupoteza maisha Aprili na Mei mwaka huo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles