24.2 C
Dar es Salaam
Monday, August 8, 2022

‘Ajali za kemikali hutokea kila siku’

Profesa Samueli Manyele
Profesa Samueli Manyele

HADIA KHAMIS NA MAULI MUYENJWA, DAR ES SALAAM

MKEMIA Mkuu wa Serikali, Profesa Samueli Manyele, amesema ajali nyingi zinazohusu matukio ya kemikali hutokea kila siku duniani kutokana na kukosekana uelewa wa matumizi sahihi na usambazaji wa kemikali hizo.

Amesema mwaka 2014 pekee zaidi ya watu 14 walifariki dunia kutokana na ajali ya kemikali zipatazo 11 ikiwamo tindikali.

Alikuwa akizungumza   Dar es Salaam jana katika ufunguzi wa mafunzo ya kuelimisha wadau juu ya matumizi sahihi na salama ya kemikali chini ya sheria za kemikali za viwandani na majumbani.

Profesa Manyele alisemawasambazaji wengi wa kemikali hawana uelewa wa kutosha kuhusiana na madhara ya kemikali hizo.

Alisema lengo la kutoa mafunzo hayo ni kuwaongezea uelewa  kuwezesha matumizi salama ya kemikali na hivyo kulinda afya na mazingira dhidi ya madhara yake.

“Bidhaa nyingi kama si zote tunazotumia katika maisha yetu ya kila siku zimetengenezwa na kemikali na viwanda vingi vinavyotengeza bidhaa hizi zinatumia maelfu ya kemikali kuzitengenezea,” alisema.

Alisema kwa ujumla kemikali hizo hutumika katika vitu vingi kama vyakula, dawa, maji na katika sehemu mbalimbali kama mahali pa kazi viwandani na mashambani.

“Ingawa kemikali zina faida nyingi katika maisha ya kila siku ya binadamu, zinaweza kuleta madhara makubwa kwa afya na mazingira kama hazitatumika katika hali ya usalama kama ilivyotakiwa, wakati wa uzalishaji, usafirishaji na matumizi mengine ya kemikali,” alisema Profesa Manyele.

Alisema kuna baadhi ya kemikali zinazotumika vibaya kama tindikali ambayo hutumika kuwadhuru watu wasiokuwa na hatia.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,235FollowersFollow
549,000SubscribersSubscribe

Latest Articles