27.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, March 21, 2023

Contact us: [email protected]

Ajali za ajabu zilizowahi kutokea duniani

AJALI si kitu cha utani au kufurahia wala kukiita cha kuchekesha kwa sababu husababisha hasara, maumivu, ulemavu hadi kifo cha kusikitisha.

Kwa mujibu wa Benki ya Dunia (WB) ajali za barabrani zinazidi kuongezeka duniani hasa katika mataifa ya Afrika, ilihusisha ongezeko hilo kuna sababu kadhaa ikiwamo kukua kwa makazi mijini.

Katika ripoti iliyotolewa na Benki ya Dunia, ilielezwa kuwa hadi kufikia mwaka huu, idadi ya vifo vinavyosababishwa na ajali za barabarani katika nchi za Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara itaongezeka kwa asilimia 80. 

Nchi hizo zina idadi kubwa zaidi ya ajali za barabarani licha ya kuwa na magari machache kuliko nchi nyingine.

Kwa mujibu wa Benki ya Dunia, inakadiriwa kwamba kwa kila wakazi 100,000 watu 24 hufa kila mwaka kwa ajali za barabarani. 

Vijana na watu maskini wako kwenye hatari kubwa zaidi. Kufikia mwaka 2025, ajali za barabarani zinatarajiwa kuwa chanzo namba moja cha vifo vya watoto wenye umri kati ya miaka mitano na 15. 

Kwa maana hiyo, ajali zitakuwa zimesababisha vifo vingi zaidi hata ya magonjwa kama malaria au Ukimwi. 

Jamii zenye watu maskini ziko hatarini zaidi kwani mara nyingi huishi kando ya barabara zenye magari mengi. 

Watoto hulazimika kupitia njia za hatari kufika shuleni na mara wanapopata ajali wanakuwa kwenye hatari kubwa zaidi ya kufa kwa sababu hawafikiwi na huduma bora za afya. 

Mbali na kusababisha majeraha, ulemavu na hata vifo, ajali zina athari za kiuchumi pia. Inakadiriwa kwamba ajali zimegharimu nchi za Kiafrika asilimia moja hadi tatu ya pato la taifa kila mwaka.

Ajali huleta majozi kwa wengi ndio maana mamlaka husika katika mataifa mbalimbali hutafuta mbinu za suluhi za kupunguza ajali kama si kuzipunguza kabisa.

Lakini pia wakati mwingine ajali zinazotokea zinaweza kuvunja mbavu kwa namna zilivyotokea katika mazingira ambayo ni vigumu kwako kuamini. 

Utakuta baada ya ajali gari limenasa katika paa kiasi cha kujiwa na wazo; imekuaje gari gari likajikuta katika paa ilihali barabara iko chini? Au liliruka kama ndege?

Nyingine utakuta gari limetoboa ukuta wa nyumba na kubakisha sehemu ya bodi ya nyuma nusu.

Picha zifuatazo ni za ajali mbalimbali zinazoweza kushangaza au kuchekesha.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
210,784FollowersFollow
563,000SubscribersSubscribe

Latest Articles