23.7 C
Dar es Salaam
Thursday, September 28, 2023

Contact us: [email protected]

Ajali yaua wawili mlima Mbalizi

ELIUD NGONDO-MBEYA

WATU wawili wamefariki dunia na wengine wawili kujeruhiwa baada ya Lori la mizigo kufeli breki mteremko wa Mlima Mbalizi katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya na kugonga watembea kwa miguu.

Akizungumza na MTANZANIA kwa njia ya Simu Mkuu wa Kikosi cha Usalama barabarani Mkoa wa Mbeya (RTO), Jumanne Mkwama alisema ajali hiyo imetokea leo jioni ambapo lori hilo lilikuwa limebeba mzigo likielekea nchi jirani ya Zambia.

Amesema watu wawili akiwemo mwendesha pikipiki maarufu kama Bodaboda walifariki papo hapo na wengine wawili ambao walikuwa wanatembea kwa mguu kujeruhiwa.

Miili ya marehemu imehifadhiwa katika Hospitali Teule ya Wilaya ya Mbeya Ifisi na majeruhi wanaendelea kupatiwa matibabu katika hospitali hiyo

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,745FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles