25.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Za hivipunde| Ajali yaua watu 19 na kujeruhi 8 Iringa

Na Raymond Minja, Mafinga

Watu 19 wamefariki dunia na wengine 8 kujeruhiwa katika ajali ya gari iliyotokea Alfajiri ya leo Ijumaa Juni 10, 2022 katika eneo la Changarawe Wilaya ya Mufindi mkoani Iring

Ajali hiyo imehusisha Lori aina ya Scania lenye namba za usajili T 736 AAE na Coaster yenye namba za usajili T 542 DQV.

Akitoa taarifa kwa Mkurugenzi wa Mji wa Mafinga, Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Mafinga, Dk. Victor Msafiri amesema ajali hiyo imesababisha vifo vya watu 19 na majeruhi ambao bado wanaendelea kupatiwa matibabu.

Amesema majeruhi wanaendelea kupata matibabu na miilii ya marehemu baadhi imeshatambulika na wengine wanaendelea kutambuliwa na jeshi la polisi.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mafinga Mji, Happiness Laizer amewatembelea majeruhi na kuwapa pole huku akiwaomba Madaktari kuwapa hudumu stahiki ili hali zao ziweze kutengemaa kwa haraka.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles