29.2 C
Dar es Salaam
Thursday, September 19, 2024

Contact us: [email protected]

Ajali yaua 11, yajeruhi 47  

Na Ramadhan Libenanga, Morogoro

WATU 11 wamefariki dunia na wengine 47 wamejeruhiwa kati yao sita wako mahututi katika ajali iliyohusisha magari matatu.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Ulrich Matei, jana aliwaambia waandishi wa habari kuwa tukio hilo lilitokea jana saa 12 jioni eneo la Dumila, pembezoni mwa kibao cha Shule ya Sekondari Dakawa lililopo Wilaya ya Kilosa barabara ya Morogoro kwenda Dodoma baada ya magari hayo matatu kugongana uso kwa uso.

Alisema katika ajali hiyo watu watatu waliungua hadi kuteketea kwa moto uliosababishwa na ajali hiyo.

Kamanda Matei alisema ajali hiyo ilihusisha gari aina ya fuso lenye namba za usajili T 963 BLW, lori la mafuta ambalo namba zake hazijafahamika kwa sababu liliteketea kwa moto.

Alisema baada ya kutokea kwa ajali hiyo, gari jingine ambalo ni basi la abiria la OTTA CLASSIC lenye namba za usajili T 201 DGK linalofanya safari zake kati ya Dar es Salaam na Kagera liligonga lori la mafuta lililokuwa limegongana na fuso na kusababisha liwake moto.

Kamanda huyo alisema ajali hiyo ya pili ilitokea saa 10 usiku katika  eneo hilo hilo na kusababisha vifo vya watu sita na majeruhi  47 kati yao sita wako mahututi.

Aliwataja waliopoteza maisha kuwa ni dereva wa basi la Kampuni ya Otta, Yasin Mgongolwa, kondakta wake, Veronica Jeremia. Wengine ni abiria waliotambuliwa kuwa ni Liliani Paul, Jonia Kokumbaga, Said Shomar na maiti ya mtu mmoja mwanamke ambaye jina halijafahamika.

“Katika ajali hii watu 47 walijeruhiwa na walipekekwa Hospitali ya Mkoa wa Morogoro wanakoendelea kupatiwa matibabu.

Kamanda Matei alisema uchunguzi wa awali wa makachero wa polisi umeonyesha kuwa chanzo cha ajali hiyo ni gari ndogo iliyokuwa mbele kusimama ghafla na kusababisha lori la mafuta kugongana na fuso.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles