22.2 C
Dar es Salaam
Thursday, August 11, 2022

Ajali yampa ushindi Pantano hatua ya 15

Jarlinson Pantano
Jarlinson Pantano

BOUR EN BRESSE, UFARANSA

NYOTA wa mbio za baiskeli katika mashindano ya Tour de France, Jarlinson Pantano, amefanikiwa kushinda hatua ya 15 ya michuano hiyo baada ya wapinzani wake 30 kuanguka.

Mbio hizo ambazo zilikuwa zinafanyika kwenye mji wa Bour en Bresse, Pantano alishinda hatua hiyo baada ya ajali ambayo ilitokea na kusababisha waendesha baiskeli 30 kuanguka hivyo kumfanya Pantano awapite na kushinda hatua hiyo.

Hata hivyo, mshindi huyo alidai kwamba hakuwa na uhakika wa kushinda kwa kuwa tayari alikuwa ameachwa nyuma huku akiamini kuwa Chris Froome angeweza kushinda.

Hata hivyo, Froome ambaye alishinda kwenye hatua ya tisa, juzi alishindwa kuwika japokuwa aliachwa nyuma kwa dakika tatu, ila inadaiwa angeweza kufanya vizuri bila ajali kutokea.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,415FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles