28.7 C
Dar es Salaam
Sunday, November 28, 2021

Ajali ya pikipiki yaua watatu

NA AMON MTEGARUVUMA

MWENDESHA pikipiki, James Kumburu (30) mkazi wa Kigonsera wilayani Mbinga mkoani Ruvuma na abiria wake wawili, wamefariki dunia papo hapo, baada ya pikipiki aliyokuwa akiendesha kugonga gari kwa nyuma lililokuwa limeegeshwa kando kando ya barabara.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, Simon Maigwa aliwataja wengine waliofariki dunia, kuwa ni Omar  Komba(26) mkazi wa Mbinga mjini na Simprosia Mbawala (36) mkazi wa Kijiji cha Kigonsera ambao walikuwa abiria.

Alisema tukio hilo, lilitokea Machi 22, mwaka huu, saa 2 usiku Kijiji cha Kiamili barabara ya Songea kwenda Mbinga.

Alisema pikipiki yenye namba za usajili MC 119 CCF aina ya Haojue iliyokuwa ikiendeshwa na Kumburu, iliigonga gari kwa nyuma lenye namba za usajili T-757 BVE aina ya Mitisubishi Fusso.

Alisema miili ya marehemu imehifadhiwa kituo cha afya Kigonsera, ambapo baadae ndugu wa marehemu walikabidhiwa kwa taratibu nyingine za mazishi.

Alisema chanzo cha ajali hiyo, ni uzembe wa dereva wa gari ambaye alishindwa kuweka alama za tahadhari na pia uzembe wa mwendesha bodaboda ambaye alikuwa anaendesha mwendo kasi bila kuchukua tahadhari.

Alisema dereva wa gari lililosababisha ajali ambaye jina lake limehifadhiwa, anashikiliwa na polisi kwa mahojiano zaidi.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,206FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles