AJALI YA PIKIPIKI YAMWACHANISHA QUEEN LATIFAH NA POMBE

0
573

NEW YORK, MAREKANI


NYOTA wa muziki wa hip hop nchini Marekani, Dana OwensQueen Latifah’, ametangaza kuachana na unywaji wa pombe pamoja na matumizi ya dawa za kulevya, baada ya kaka yake kupoteza maisha kwa ajali ya pikipiki.

Kaka yake huyo anajulikana kwa jina la Lancelot Jr, amefariki dunia baada ya kupata ajali mbaya alipokuwa akiendesha pikipiki aliyonunuliwa na dada yake ambaye ni Queen Latifah.

Kutokana na kitendo hicho cha kumpoteza kaka yake, Queen Latifah ametangaza kuachana na matumizi ya pombe na dawa za kulevya.

“Nimempoteza mtu muhimu sana katika maisha yangu, alikuwa na mchango mkubwa kwenye kazi zangu, alikuwa ananipenda sana, siwezi kuwa na hasira kwa Mungu kwa kuwa yeye ndiye kila kitu kwetu na ameamua kufanya alichopanga.

“Kila kitu kinatokea kwa sababu zake na kwa sasa naachana na matumizi ya dawa za kulevya pamoja na pombe na namrudia Mungu wangu,” alisema Queen Latifah.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here