30.9 C
Dar es Salaam
Monday, October 2, 2023

Contact us: [email protected]

Ajali ya lori yaua watatu, yajeruhi 19

Mayala Towo,
Mayala Towo,

NA RAMADHAN HASSAN, DODOMA

WATU watatu wamefariki dunia na wengine saba kujeruhiwa vibaya katika ajali ya lori iliyotokea katika Kijiji cha Chifutuka, Wilaya ya Bahi, mkoani hapa.

Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo, Mrakibu Mwandamizi wa Jeshi la Polisi, Mkoa wa Dodoma, Mayala Towo, alisema lori hilo lenye namba za usajili T 689 BEG, lilikuwa likitoka katika mnada wa Mgaga likiwa limebeba watu na mizigo.

Kwa mujibu wa Mayala, kabla ya ajali hiyo, lori hilo lilichomoka tairi la mbele na kupinduka.

“Gari hilo lilichomoka tairi ya mbele na kupinduka, kisha mizigo ikawalalia abiria waliokuwamo.

“Kwa hiyo, abiria watatu walifariki papo hapo na wengine 19 wamejeruhiwa wakiwamo saba waliolazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma,” alisema.

Naye Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo, Dk. Zainabu Chaula, alisema walipokea majeruhi 19 pamoja na maiti watatu.

“Maiti tulizopokea ni za Izdori Thomas (38), Michael Msongela (29) na Elias Masimo (51), wote wakazi wa Dodoma.

“Majeruhi tuliowapokea walikuwa ni 19, lakini 12 kati yao walitibiwa na kuruhusiwa na waliobaki tumewalaza katika wodi namba nane, 10 na 11,” alisma Dk. Chaula.

Aliwataja waliolazwa kuwa ni Muoni Magege (40), mkazi wa Dar es Salaam, Suzy Samweli (16) Frida Chipaga, Chausiku Mohammed (38), Josephine Sakiru (43) Seleman Salum (35) na Elias Petro(51) wote wakazi wa Dodoma.

Akisimulia ajali hiyo mmoja wa majeruhi ambaye amelazwa katika wodi namba nane, (Chausiku Mohammed), mkazi wa Chinangali, alisema anachokumbuka ni kwamba aliona tairi likichomoka kisha akapoteza fahamu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
575,000SubscribersSubscribe

Latest Articles