29.6 C
Dar es Salaam
Sunday, October 1, 2023

Contact us: [email protected]

Ajali ya basi yaua watu 4 Songwe, 35 wajeruhiwa

Na Denis Sinkonde, Songwe

Watu wanne wamefariki na wengine 35 kujeruhiwa katika ajali ya basi la Kilimanjaro Express lililokuwa linatoka Tunduma kwenda Dar es Salaam asubuhi ya Machi 14, 2022 eneo la Senjele wilayani Mbozi Mkoa wa Songwe.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe, Rashid Ngonyani amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba taarifa za awali zinaonyesha watu wanne wamefariki dunia

Amesema taarifa chanzo cha ajali hiyo ni atatoa taarifa hiyo baada ya kukamilika uchunguzi.

Kamanda Ngonyani amesema majeruhi wamepelekwa hospitali kwa matibabu wakati miili ya marehemu imehifadhiwa hospitali ya Vwawa iliyopo wilayani Mbozi.

Ajali hiyo inatokea siku chache baada ya watu watatu kufariki dunia na wengine wawili kujeruhiwa katika ajali nyingine iliyohusisha lori la mafuta na gari dogo

Baadhi ya mashuhuda wa ajali hiyo wamesema basi hilo limeanguka baada ya kushindwa kulipita lori eneo dogo alilokuwa akilazinisha dereva wa basi na basi hilo limetumbukia kwenye korongo baada kuviringika mara kadhaa na hatimaye bodi ya gari kukatika kuanzia kwenye madirisha.

Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Omary Mgumba amefika eneo la tukio na kushuhudia shughuli ya uokoaji ikiendelea na hivyo ameiomba serikali ipanue barabara hiyo kauli ambayo naye Spika wa Bunge na Mbunge wa Mbeya Mjini, Dk. Tulia Ackson amekuwa akiiomba serikali itengeneze barabara kuanzia Igawa wilayani Mbarali hadi Tunduma mkoani humo.

Aidha, wadau wa usafiri wameshauri mizigo isafirishwe kwa usafiri wa Treni (TAZARA) kupunguza malori barabara ya Dar es Salaam – Tunduma.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles