Ajali Polisi Tanzania, mchezaji avunjika miguu

0
313

Na Winfrida Mtoi, Mtanzania Digital

Timu ya Polisi Tanzania imepata ajali asubuhi ya leo wakati inatoka mazoezini kwenye Uwanja wa TPC, Moshi, jumla ya majeruhi ni 18, wachezaji 16, dereva na mwalimu msaidizi, huku mchezaji Gerald Mdamu akidaiwa kuvunjika miguu yote.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa klabu ya Polisi Tanzania, Hassan Juma, amesema majeruhi wanaendelea na matibabu katika hospitali ya KCMC , Moshi.

Juma amewataja majeruhi wengine kuwa ni Abdullazizi Mkame, Pius Buswita, Daruweshi Saliboko, Deusdedity Cosmas, Salum Ally, Abdulmaliq Adam, Idd Mobby, Marcel Kaheza, Shabani Stambuli.

Yahaya Mbegu, Datusi Peter, Mohammed Bakari,Mohammed Yusuph, Kassim Haruna, Christopher John, George Mketo (kocha msaidizi), Vicente Ngonyani (dereva).

Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa, amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema gari iliacha njia na kugonga mti na kusababisha majeruhi.

“Gari ilikuwa imebeba watu 32, wachezaji na makocha na madaktari, kuna mchezaji mmoja anaitwa Gerald Mdamu, amevinjika miguu yote na dereva amevunjika mbavu,” amesema Kamanda Maigwa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here