21.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, October 4, 2022

AIRTEL YAZINDUA ‘HAKATWI MTU HAPA’

 

Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Kampuni ya Airtel Tanzania, Beatrice Singano na Meneja Masoko wa Airtel, Isack Nchunda wakionyesha bango la uzinduzi wa huduma ya ‘Hakatwi Mtu Hapa-Tuma Pesa Bure’ jijini Dar es Salaam leo. Picha na Fidelis Felix

Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Kampuni ya Simu za Mkononi ya Airtel, imezindua huduma mpya ya kutuma na kupokea fedha kupitia Airtel Money bila makato.

Mkurugenzi wa Masoko wa kampuni hiyo, Isack Nchunda amesema hayo leo Alhamisi Julai 5, na kuongeza kuwa lengo la huduma hiyo inayojulikana kama ‘Hakatwi Mtu Hapa-Tuma Pesa Bure’ ni kuunga mkono juhudi za serikali na kuwawezesha wateja wa Airtel nchini kutuma na kupokea fedha bure.

“Mwaka jana tulizindua huduma ya kutuma na kupokea fedha bure kwa wateja wa Airtel Money wanaotuma fedha kuanzia sh 200,000 na kuendelea na sasa tumezingatia tena uhitaji wa huduma kwa wateja wetu wengi kupitia huduma hii ambayo tunaamini watakaoitumia wataifurahia.

“Tunategemea kuona wateja wakichangamkia fursa hii ya kutuma na kupokea fedha bila makato yoyote ili kuokoa fedha zaidi ya Sh 5,000 kuanzia sasa,” amesema.

Pamoja na mambo mengine, Nchunda amesema Airtel imelenga kuboresha huduma za kifedha nchini kwa kuwafikia zaidi ya asilimia 80 ya Watanzania ambao hawajafikiwa na huduma za kibenki ambapo imeunganishwa na benki zaidi ya 40 ili kurahisisha wateja kufanya mihamala mbalimbali kama vile kuhamisha fedha kutoka kwenye akaunti ya benki kwenda kwenye akaunti ya Airtel Money muda wowote.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel, Beatrice Singano amesema huduma hiyo ni rahisi na inapatikana kwenye maduka zaidi ya 50,000 ya Airtel nchi nzima.

“Kupitia huduma hii mpya, wateja wetu wataweza kuokoa zaidi ya Sh 5,000 ya kutuma fedha ambayo kwa mwananchi wa kawaida ni fedha nyingi inayotosheleza mahitaji ya siku,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,654FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles