27.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Airtel yawafikia wafanyabiashara Soko la Feri

mussa-zunguNa MWANDISHI WETU
-DAR ES SALAAM

KAMPUNI ya simu za mkononi ya Airtel kupitia mpango wake wa Airtel Fursa, imewawezesha wafanyabiashara zaidi ya 150 wa maeneo ya Magogoni katika Soko la Feri kuendesha biashara zao chini ya miavuli baada ya kampuni hiyo kuwawezesha vifaa hivyo.

Kutokana na hilo wafanyabiashara hao wamekabidhiwa miavuli ya biashara kwa lengo la kuboresha maeneo yao ya kazi.

Akikabidhi vifaa hivyo jana jijini Dar es Salaam, Mbunge wa Ilala, Mussa Zungu (CCM), alisema amefarijika kwa hatua ya Airtel Tanzania kuwapa vifaa hivyo wafanyabiashara hao ambao wapo katika jimbo lake.

“Nafurahi kuona Airtel wamejitoa kuwasaidia wafanyabiashara hawa kuendesha biashara zao, msaada huu unathibitisha dhamira ya Airtel ya kuwawezesha wajasiriamali wadogo wadogo kuendesha biashara zao ili kukuza kipato na kuinua maisha yao.

“Miavuli inayotolewa na Airtel leo (jana) itawasaidia wafanyabiashara hawa kujikinga na jua kali la Dar es Salaam na wakati mwingine mvua. Nachukua fursa hii kuwapongeza Airtel kwa juhudi zao mbalimbali katika kuwasaidia wafanyabiashara kupitia programu yao ya Airtel Fursa,” alisema.

Mbunge huyo alitoa wito kwa makampuni mengine kuiga mfano huo kwani hata kwa kiasi kidogo watakachotoa watakuwa wameweza kusaidia wajasiriamali hao ambao wamekuwa wakihangaika kukuza kipato chao.

Kwa upande wake Meneja Huduma kwa Jamii, Hawa Bayumi, alisema: “Airtel ni kampuni inayoamini katika kusaidia jamii katika maeneo tunayoendesha biashara zetu.

Kwa kupitia mpango wa Airtel Fursa kwa mara nyingine tunatoa msaada kwa wafanyabiashara wa wadogo wadogo Kivukoni kwani tunaamini mtu yeyote anaweza kufanya biashara pale atakapowezeshwa.

“Kupewa motisha na pindi yeye mwenyewe atakapokuwa na nia thabiti, kujituma na malengo sambamba na nidhamu katika kazi,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles