27.5 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

AIBU VIONGOZI KUZUNGUMZA NA WAZAZI JUU YA USAJILI WA WACHEZAJI

Na JENNIFER ULLEMBO-DAR ES SALAAM

TAYARI mchakato wa usajili umezidi kushika kasi kwa klabu mbalimbali hapa nyumbani, lakini zile zinazosikika hasa zinatokea Ligi Kuu Tanzania Bara.

Ikiwa ni wiki chache zimepita tangu kumalizika kwa msimu wa ligi 2016/2017, timu mbalimbali zimeshuhudiwa zikikamilisha usajili kwa kunasa saini za wachezaji mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi.

Lakini hiki kinachoendelea sasa kinashangaza, timu inafanya mazungumzo ya awali na mchezaji na kuishia naye njiani (kuachana naye bila kufikia mwafaka).

Tabia hii imekuwa ikifanywa na timu zinazojiita wakongwe katika ligi, hiyo imekuwa ikisababishwa na uelewa mdogo wa wachezaji na tamaa ya kutaka kuona wakichezea klabu hizo zenye majina.

Mwenendo huu haujaanza kipindi hiki, bali ni kama mwendelezo wa kile kilichoanzisha misimu mitano au sita iliyopita huko nyuma.

Hapa ndipo zinapozalishwa kesi za mchezaji kusajili kwenye timu mbili tofauti ndani ya muda mfupi, klabu moja kuibiwa mchezaji na nyingine.

Ukweli halisi hivi sasa soka limezidi kupiga hatua na mabadiliko mengi yamekuwa yakitokea, hivyo ni vema viongozi husika wa klabu na timu wakalitambua hili.

Kauli ambazo zimekuwa zikisikika mara kwa mara, pindi viongozi wa timu flani wanapotaka kufanya usajili na kuona mbinu zao zinakwama ni kuwa ‘subiri tukazungumze na wazazi wake’ ili akubali kuichezea timu husika.

Aibu tena ni aibu kubwa, tunashindwa kujifunza kutoka kwa mataifa ambayo yamepiga hatua, haijawahi kusikika hata siku moja vigogo wa Man United, Arsenal, Chelsea wakijiandaa kuzungumza na wazazi wa wachezaji wanaowataka ili waingie nao mikataba.

Aibu kubwa Tanzania tutafika kweli, sisi ambao tunahitaji kuona nchi yetu ikipiga hatua kutoka hapa tulipo na kufika kule, kwa kushirikisha wazazi sababu tu ya ukaribu na urafiki.

Haya yamekuwa yakishuhudia katika jamii ya Kitanzania, lakini upande wa ndoa ‘wazazi kumchagulia mtoto mume au mke wanayemtaka wao na kulazimisha ndoa hiyo kufungwa’.

Wachezaji wanaocheza Ligi Kuu hata wale wa Ligi Daraja la Kwanza ni watu wazima wanaojitambua na kufahamu kitu gani kizuri na kibaya, hivyo viongozi acheni tabia ya kuendesha soka kizamani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles