25.2 C
Dar es Salaam
Monday, December 2, 2024

Contact us: [email protected]

AHUKUMIWA MIAKA MIWILI JELA KWA KUKEKETA MTOTO

new-law

Na TIMOTHY ITEMBE – TARIME

MKAZI wa Kijiji cha Itiryo, Kata ya Itiryo, Wilaya ya Tarime mkoani Mara, Angelina Charles (50), amehukumiwa kwenda jela miaka miwili kwa kosa la kumkeketa binti wa miaka 14.

Akimsomea mashtaka mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Mahakama ya Wilaya ya Tarime, Matha Mpaze, Mwendesha Mashtaka wa Polisi, Neema Antony,  alisema kuwa mshtakwa alitenda kosa hilo Desemba 7, mwaka huu kijijini hapo.

Alidai kuwa baada ya mshtakiwa kufikishwa mahakamani Desemba 14, mwaka huu alikiri kuhusika kumkeketa binti huyo ambaye ni mtoto wa mdogo wake, huku upande wa mashtaka ukitoa kielelezo cha PF3.

Baada ya maelezo hayo, Hakimu Mpaze alimtia hatiani mtuhumiwa na kumhukumu kwenda jela miaka miwili au kulipa faini ya Sh 500,000. Hakuweza kulipa faini na kupelekwa gerezani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles