27.1 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

AHMADINEJAD KUWANIA URAIS LRAN

TEHRAN, IRAN


RAIS wa zamani wa Iran, Mahmoud Ahmadinejad, amejiandikisha kuwa mgombea wa kiti cha urais kwenye uchaguzi mkuu nchini humo, licha ya kuonywa na Mahakama Kuu kutogombea.

Ahmadinejad, mwenye msimamo mkali na ambaye alihudumu kama rais kwa mihula miwili mwaka 2005 hadi 2013, aliwasilisha fomu makao makuu ya Wizara ya Mambo ya Ndani kuwania kiti cha urais katika uchaguzi utakaofanyika Mei 19.

Mwaka jana, Ayatollah Ali Khamenei alimuonya kuwa hatua kama hiyo ‘haina masilahi kwake wala taifa’.

Lakini Ahmadinejad amewaambia wanahabari kuwa hilo lilikuwa kama ‘ushauri tu’.

Waandishi walimshuhudia Ahmadinejad akijiandikisha siku ya Jumanne, na walisema maofisa wa uchaguzi walishangaa walipomuona akiwasilisha fomu hizo.

Rais Hassan Rouhani, mwanasiasa mwenye msimamo wa kadiri na ambaye alihusika katika kupatikana mwafaka kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran na viongozi wa mataifa yenye nguvu duniani mwaka 2015, bado hajawasilisha fomu, lakini anatazamiwa na wengi kugombea tena urais kwa muhula wa pili.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles