26.2 C
Dar es Salaam
Sunday, August 14, 2022

Agnieszka atwaa taji la China Open

agnieszka-radwanskaBEIJING, CHINA

NYOTA wa mchezo wa tenisi nchini Polish, Agnieszka Radwanska, ametwaa taji la China Open baada ya kumchapa mpinzani wake, Johanna Konta kwa seti 6-4, 6-2.

Katika fainali hiyo ambayo ilipigwa juzi jijini Beijing nchini China, mashabiki wengi walimpa nafasi Johanna kutokana na mchezo ambao aliuonesha katika nusu fainali, lakini katika fainali hiyo alikutana na mpinzani ambaye alikuwa na uwezo zaidi.

Japokuwa Johanna amepoteza katika fainali hiyo, lakini bado yupo katika nafasi 10 bora kwa wachezaji wa tenisi duniani kwa upande wa wanawake.

Johanna anashikilia nafasi ya kwanza kwa ubora katika mchezo huo kwa upande wa wanawake nchini Uingereza, wakati mpinzani ambaye ametwaa taji hilo, anashika nafasi ya tatu kwa ubora duniani.

Kwa upande wa Agnieszka, amedai kuwa hakuwa na uhakika kama angeweza kushinda fainali hizo kutokana na ugumu wa safari yake kwenye michuano hiyo ambayo imemalizika.

“Ninaamini kila kitu kimekwenda sawa, nimekuwa na furaha kubwa kutokana na kile ambacho nimekifanya, ukweli ni kwamba ushindani ulikuwa mkubwa sana, lakini nashukuru nimeweza kufanikiwa na kutimiza malengo yangu.

“Ushindani ulikuwa mkubwa sana kutokana na maandalizi ambayo yalifanyika kwa washiriki wote, sikuwa na uhakika kama ningefika hapa, lakini nashukuru kuwa nimeweza kutimiza malengo yangu,” alisema Agnieszka.

Kwa upande wa Johanna, naye amedai kuwa amefurahishwa na kiwango cha mpinzani wake kwa kuwa aliweza kutumia mapungufu ya upande wa pili na kumfanya awe bingwa.

“Katika mchezo huu siku zote mshindi anakuwa mmoja, nilijiandaa vizuri kuhakikisha nachukua ubingwa, lakini kuna makosa ambayo niliyafanya na mpinzani wangu akaweza kutumia nafasi hiyo.

“Alionesha kiwango kizuri na ndio maana amefanikiwa kutwaa ubingwa, kikubwa kilichobaki ni kuyafanyia kazi makosa niliyoyafanya ili kuweza kufanya vizuri katika michuano ijayo,” alisema Johanna.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,656FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles