22.2 C
Dar es Salaam
Monday, October 18, 2021

AGNES MASOGANGE AJISALIMISHA MAHAKAMANI

Na KULWA MZEE – DAR ES SALAAM

MREMBO anayepamba video za wasanii mbalimbali wa Bongo Fleva, Agnes Gerald maarufu Masogange (28), ambaye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ilitoa hati akamatwe kwa kushindwa kuhudhuria kwenye kesi inayomkabili ya kutumia dawa za kulevya, amejisalimisha mwenyewe mahakamani hapo.

Masogange alijisalimisha jana asubuhi kabla ya kesi mbalimbali kuanza kusikilizwa mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbroad Mashauri.

Awali mahakama ilitoa hati ya kukamatwa kwa Masogange baada ya upande wa mashtaka kuomba mahakama kutoa hati hiyo kutokana na mshtakiwa huyo na wadhamini wake kutofika mahakamani mara mbili licha ya kupewa onyo.

Akiiwakilisha Jamhuri, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Shadrack Kimaro, alidai mahakamani hapo kwamba upelelezi wa kesi hiyo umekamilika hivyo wanaomba tarehe nyingine ya kumsomea mshtakiwa maelezo ya awali.

Hakimu Mashauri aliahirisha kesi hiyo hadi Mei 13, mwaka huu kwa ajili ya kusomwa maelezo ya awali dhidi ya mashtaka yanayomkabili mtuhumiwa ambaye ni Masogange.

Masogange anakabiliwa na mashtaka ya kutumia dawa za kulevya aina ya heroin diacety na Oxazepam.

Katika kesi hiyo namba 77 ya mwaka huu, Masogange anadaiwa kuwa kati ya Februari 7 na 14, mwaka huu, katika maeneo yasiyojulikana ndani ya Jiji la Dar es Salaam, alitumia dawa za kulevya aina ya Heroin (Diacety Imophine) na Oxazepam, jambo ambalo ni kinyume na sheria.

Hata hivyo, Masogange alikana mashtaka hayo na yupo nje kwa dhamana.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
162,220FollowersFollow
521,000SubscribersSubscribe

Latest Articles