24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Agizo la Lugola laanza kutekelezwa

Na RAMADHAN HASSAN-DODOMA

TAASISIi mbalimbali za Serikali zimekutana  Dodoma  kufanya mazungumzo ya awali  kutekeleza agizo la Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola kuwa pikipiki zote zinazotumika kusafirisha abiria zifungwe tela,  ikiwa ni mkakati  wa kupunguza ajali.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Jacob Kingu alikuwa akizungumza  jijini hapa jana wakati wa maonyesho ya  pikipiki ya mfano yenye tela zinazotengenezwa na Shirika la Mzinga.

Alisema  serikali imedhamiria kuondoa na kukomesha ajali za bodaboda   na kulinda usalama wa watumiaji wa usafiri huo.

Alisema wizara yake kwa kushirikiana na wadau wengine kutoka taasisi za serikali, Shirika la Mzinga, Mamlaka ya Elimu na Ufundi Stadi(Veta), Shirika la Viwango Tanzania(TBS),  Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo(Sido), Kiwanda cha Kutengeneza Magari (Nnyumbu) na Jeshi la Polisi zitahakikisha zinakuwa na mpango wa pamoja wa kuratibu na kuhakikisha mkakati huo utakaosaidia kupunguza ajali unakamilika.

“Leo (jana) tumekutana hapa kujadili jinsi ya kuliendea jambo hili la kufunga tela.

“Kamati ya  wataalamu hawa ndiyo itakutana na kuratibu andiko ambalo litapelekwa  kwa viongozi wa wizara mbalimbali zinazohusika na suala la kudhibiti ajali za barabarani na kumlinda mtumiaji wa huduma ya usafiri huo,” alisema Meja Jenerali Kingu.

Aliwataka wananchi wawe na subira kipindi hiki ambacho kamati hiyo ya wataalamu inaenda kuandaa mpango huo na mapema mwishoni mwa mwaka huu mpango huo utatangazwa .

Akizungumzia pikipiki hiyo ya mfano yenye tela, Mtaalamu kutoka Shirika la Mzinga,  Salum Kipande alisema pikipiki hiyo imetengenezwa vizuri na itakua na uwezo wa kubeba abiria wanne na dereva mmoja.

Mtaalamu huyo alisema wanaendelea kuunga mkono azma  ya serikali kupunguza ajali za bodaboda nchini kwa kutengeneza pikipiki hizo kwa ustadi.

Kaimu Mkurugenzi Elimu na Mafunzo wa Mamlaka ya Elimu na Ufundi Stadi (VETA), Stella Ndimubenya,  alisema wao kama VETA watahakikisha wanatumia teknolojia waliyonayo kuweka kifaa maalumu ambacho kitadhibiti upakiaji wa abiria kupita kiwango.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles