33.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

AGIZO LA JPM LAWANUFAISHA MACHINGA SENGEREMA

Na BENJAMIN MASESE               |              


SIKU chache baada ya Rais Dk. John Magufuli kuagiza  uongozi wa Mkoa wa Mwanza   kushughulikia  haraka malalamiko ya wafanyabiashara wadogo  (machinga) wanaonyang’anywa bidhaa zao wilayani Sengerema,imeelezwa kuwa    watalipwa fidia leo.

Rais  Magufuli  alitoa agizo hilo  Agosti 18, mwaka huu baada ya kupita Wilaya ya Sengerema akienda  Wilaya ya Chato kwa ajili ya mapumuziko.

Alisimama   kuwasalimia wananchi ndipo wamachinga  walipomweleza jinsi walivyonyang’anywa bidhaa zao.

Mmoja wa machinga hao, Jocob Mlinga alisema Agosti 10, mwaka huu  ilifanyika operesheni ya kuwaondoa wafanyabiashara wadogo ambako  wote waliokuwa wamepanga bidhaa zao kandokando ya  barabara  walinyang’anywa.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongela, juzi alipiga kambi wilayani Serengerema   kwa lengo la kutekeleza agizo la Rais Magufuli ambako ilibainika   wafanyabiashara 11 wa   mananasi  walichukuliwa bidhaa zao.

Mongela alimwagiza  Mkurugenzi  Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema, Magesa Boniface kuwalipa fidia machinga hao 11 leo.

Pia alimwagiza  kulifanyia marekebisho soko lililipo karibu na eneo wanalouzia mananasi    kwa kujenga mabanda ya nguzo za mabomba yatakayoezekwa  kwa mabati  kuwatengenezea kivuli.

Alisema  baada ya hapo wafanyabiashara hao washirikishwe katika kupanga na kuhamia katika eneo hilo.

“Kuanzia leo Jumatatu (juzi)  nakuagiza wewe mkurugenzi kwa kusaidiana na Mkuu wa Wilaya, Emmanuel Kipole anzeni kuandaa utaratibu wa kuwalipa fidia wale waliochukuliwa mananasu yao.

“Ifikapo Agosti 22, hatua hiyo iwe imekamilika, kila mmoja atasema kiasi cha matunda yaliyochukuliwa.

“Rais Magufuli ameagiza nishughulikie tatizo hilo na kupata suluhu, sasa nami nakuagiza   kuwalipa fidia na kuwaboreshea soko ili wahamie pale.

“Baada ya hapo hatutaki tena kuwaona kandakando ya barabara,”alisema Mongela.

RC vilevile   alimwelekeza  mkurugenzi   kuwa maofisa maendeleo ya jamii watumike kwenda kwenye jamii kuwaelewesha   wananchi  kuhusu umuhimu wa masuala  mbalimbali yenye tija  na  si watu  wa mapato ambao kazi yao ni kukusanya mapato.

Mmmoja wa wamachinga,   Jacob Mlinga alimweleza Mongela kwamba alichukuliwa mananasi yake 700 yaliyokuwa kwenye matoroli mawili.

Mfanyabiashara mwingine, Elina Taibu anayejishughukisha na biashara ya urembo alimshukuru Rais  Magufuli kwa kuwajali wanyonge na kuomba kuendelea kuwatetea na kushughulikia matatizo ya watu wa chini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles