AFYA YA RICK ROSS YAKAA SAWA

0
637

MIAMI, MAREKANI


RAPA Rick Ross, ameweka wazi kuwa afya yake kwa sasa imekaa sawa na yupo tayari kwa ajili ya kuendelea na matamasha mbalimbali.

Mkali huyo wa ‘Aston Martin Music’, wiki chache zilizopita alikuwa anahudhuria hospitalini mara kwa mara kutokana na kusumbuliwa na tatizo la upumuaji, tatizo hilo lilianza kugundulika tangu Machi mwaka huu.

Baada ya kupata huduma kwa kipindi hicho chote ambacho kilimfanya ashindwe kufanya baadhi ya matamasha, ameweka wazi kuwa yupo tayari kwa ajili ya kuwapa burudani mashabiki wake.

“Nimerudi katika afya bora, nipo tayari kwa ajili ya kuwapa burudani mashabiki wangu baada ya kushindwa kufanya hivyo kwa kipindi cha wiki kadhaa, lakini sasa ninawahakikishia kuwa nipo tayari kuwapa mashabiki zangu kile ambacho walikuwa wanakikosa, pia ninawashukuru kwa sapoti,” alisema Rick Ross.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here