30.8 C
Dar es Salaam
Saturday, January 28, 2023

Contact us: [email protected]

AFYA YA MANJI YAIMARIKA

NA VERONICA ROMWALD

-DAR ES SALAAM

AFYA ya Mfanyabiashara Yusuph Manji ambaye amelazwa  katika Taasisi ya Tiba ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), anakopatiwa tiba ya ugonjwa wa moyo akiwa chini ya uangalizi wa polisi, inazidi kuimarika.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano JKCI, Anna Nkinda amesema kutokana na afya ya mfanyabiashara huyo ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Mbagala, kuzidi kuimarika madaktari wakiridhia anaweza kuruhusiwa wakati wowote.

Manji alilazwa hospitalini hapo kwa mara ya pili Februari 16, mwaka huu, baada ya kupata dhamana katika ya kesi inayomkabili katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, akituhumiwa kutumia dawa za kulevya.

Awali alifikishwa hospitalini hapo Februari 12, mwaka huu baada ya kuugua ghafla akiwa katika Kituo Kikuu cha Polisi jijini Dar es Salaam alikokuwa anashikiliwa kwa mahojiano tangu Februari 9, mwaka huu baada ya kutajwa katika orodha ya watu wanaojihusisha na dawa za kulevya iliyotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,063FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles