25.3 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 29, 2022

Contact us: [email protected]

Afrika Mashariki haimo kwenye viwango vya warefu

Na SMITHA MUNDASAD MWANDISHI WA HABARI ZA AFYA

LISHE duni kwa watoto wenye umri wa kwenda shule inaweza kuchangia pengo la urefu wa wastani wa sentimita 20 

katika ya mataifa yenye watu warefu na wafupi, uchambuzi unaonyesha. 

Inaripotiwa kuwa kwa mwaka 2019 mtoto wa kiume mrefu zaidi ni yule wa miaka 19 aliyekuwa anaishi nchini Uholanzi.

Kijana huyo alikuwa na urefu wa futi sita (183.8cm au 6ft) na mfupi kabisa alikuwa anaishi Timor Leste ambaye alikuwa na futi tano na inchi tatu  (160.1cm au 5ft 3in).

Katika hatua nyingine kiwango cha urefu nchini Uingereza kimeshuka kwenye rekodi za dunia, kwani kijana mrefu zaidi nchini humo mwenye miaka 19 ameshika nafasi ya 39 katika mwaka 2019  akiwa na futi tano na inchi 10  (1.78m au 5ft 10in) Uingereza imeshuka kutoka nafasi ya 28 mwaka 1985.

Watafiti wanasema kufuatilia mabadiliko katika urefu na uzito wa watoto ulimwenguni kote na kwa muda ni muhimu kwa sababu wanaweza kuonyesha ubora wa lishe inayopatikana, na jinsi mazingira ya afya yanavyokuwa kwa vijana.

Timu ilichambua data kutoka kwa zaidi ya watoto milioni 65 na vijana wenye umri wa miaka 5 hadi 19 kutoka katika tafiti zaidi ya 2000 kati ya mwaka 1985 na 2019.

Waligundua kuwa katika mwaka 2019, kwa wastani, watoto na vijana kaskazini magharibi na katikati ya Ulaya (kwa mfano wale wa Uholanzi na Montenegro) walikuwa warefu zaidi ulimwenguni.

Wakati huo huo, watoto wa miaka 19 ambao kwa wastani walikuwa wafupi zaidi waliishi Kusini na Kusini-Mashariki mwa Asia, Amerika Kusini na Afrika Mashariki.

Kwa wastani uchambuzi unaonyesha kijana wa kiume wa miaka 19 wa Laos  alikuwa na urefu  wa 162.8cm au 5ft 4in saa na mtoto wa kiume wa miaka  13 wa nchini Uholanzi.

Msichana wa miaka 19  wa Guatemala, Bangladesh, Nepal na Timor Leste  alikuwa na urefu sawa na mtoto wa kike wa miaka 11 wa Uholanzi mwenye urefu wa 152cm au 5ft).

Nchini Uingereza kijana wa kiume wa miaka 19 alikuwa na urefu wa 178.2cm (5ft 10in), na msichana 163.9cm (5ft 5in).

Mabadiliko makubwa ya urefu kwa watoto kwa zaidi ya miaka 35 yameonekana China na Korea Kusini.

Lakini katika nchi nyingi za Afrika Kusini mwa jangwa la Sahara,wastani wa urefu  haujabadilika au umepungua tangu mwaka 1985.

Utafiti pia uliangalia uzito wa watoto, kipimo ambacho kinaonyesha kama ana afya kulingana na urefu wake.

Watafiti walibaini  kuwa vijana wenye uzito mkubwa wanaishi visiwa vya Pacific, Mashariki ya kati, Marekani na New Zealand.

Wakati vijana wenye miaka 19 wenye uzito mdogo wanaishi Asia Kusini kama India na Bangladesh.

Watafiti wanakadiria kuwa tofauti ya nchi kwenye uzito mdogo na mkubwa ni kilogramu 25.

Katika baadhi ya nchi watoto wamefikia kiwango cha uzito wenye afya wakiwa na miaka mitano, lakini walionekana kuelekea kupata uzito mkubwa wakati watakapotimiza miaka 19.

Wakati watafiti wanakubali kwamba maumbile huchukua sehemu muhimu katika urefu na uzito wa watoto, wanasema linapokuja suala la afya ya watu wote, lishe na mazingira ni muhimu.

Wanasema pia kwamba sera za lishe ulimwenguni huzingatia sana watoto chini ya miaka mitano, lakini wanapendekeza utafiti wao unaonyesha umakini zaidi unahitajika katika mifumo ya ukuaji wa watoto wakubwa.

Dk. Andrea Rodriguez Martinez kutoka chuo cha Imperial London, mmoja wa watafiti walioongoza utafiti huo alisema uzani mzuri na urefu katika utoto na ujana una faida ya maisha kwa ustawi wa watu.

Alisema: “Matokeo yetu yanapaswa kuhamasisha sera zinazoongeza upatikanaji na kupunguza gharama ya vyakula vyenye lishe, kwani hii itasaidia watoto kukua kwa urefu bila kupata uzito kupita kiasi kwa urefu wao

“juhudi hizo ni pamoja na kutoa vocha za chakula kwa familia zenye kipato cha chini, na chakula cha bure cha shuleni.”

Wakati huo huo, Prof Alan Dangour, kutoka London School of Hygiene and Tropical Medicine, alisema ulikuwa uchambuzi wa kipekee na wenye nguvu.

Aliongeza: “Kwa mara ya kwanza, uchambuzi huu wa ulimwengu umezingatia ukuaji wa watoto walio na umri wa kwenda shule na vijana, na kubainisha kwamba serikali ulimwenguni hazifanyi vya kutosha kuhakikisha kuwa watoto wanaingia watu wazima wakiwa na afya njema.”

Habari hii imetafsiriwa kutoka Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC).

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
205,454FollowersFollow
558,000SubscribersSubscribe

Latest Articles