22.2 C
Dar es Salaam
Saturday, August 20, 2022

AFRIKA KUSINI: Serikali kukutana na mabalozi kujadili mashambulizi dhidi ya wageni

Waziri wa Maswala ya Kigeni nchini Afrika Kusini ameitisha mkutano wa dharura na mabalozi kufuatia mashambulizi dhidi ya wageni mjini Durban.

Mapema Jumatatu watu watatu walifariki kufuatia maandamano yanayolenga maduka, mengi ambayo yanamilikiwa na wageni.

Takriban watu 50 walitafuta hifadhi katika kituo kimoja cha polisi wakati kundi moja la vijana wa Afrika wasio na kazi walipowashinikiza kutoka katika majumba yao usiku.

Wageni wanalengwa na watu ambapo wanawashtumu kuchukua kazi zao.

Wiki iliopita , makumi ya raia walilazimika kutoka katika nyumba zao na waandamanaji waliojawa na hasira ambao pia waliwaibia maduka yao.

Wakati huohuo Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa ameshtumu ghasia za hivi karibuni za mashambulizi dhidi ya wageni na kutoa wito kwa taasisi za kiusalama kuwakamata wanaotekeleza vitendo hivyo.

Amesema kuwa ghasia hizo, ambazo zimekuwa zikiwalenga raia wa Malawi na raia wengi wa Afrika katika jimbo la Kwazulu Natal ni swala la kujutia hususan katika mkesha wa siku ya mwezi wa uhuru ambapo taifa hilo linaadhimisha miaka 25 tangu uchaguzi wa kidemokrasia nchini humo.

”Leo uchumi wetu na faida za jamii yetu zinatokana na biashara na uwekezaji kutoka kwa washirika wetu katika bara Afrika na wengi wanaishi hapa nchini Afrika Kusini ambapo wanachangia pakubwa maenedeleo ya taifa hili. Maendeleo ya Afrika yanatokana na ongezeko la watu na mizigo kutoka eneo moja hadi jingine kati ya mataifa tofauti ili sote tuweze kufaidika, hatutakubali kuwawacha wahalifu kurudisha nyuma hatua zilizopigwa”.

Wiki iliopita, makumi ya raia walilazimika kutoka katika nyumba zao na waandamanaji waliojawa na hasira ambao pia waliwaibia maduka yao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
199,057FollowersFollow
551,000SubscribersSubscribe

Latest Articles