23.9 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

AFRIKA KUSINI KUIUZIA IRAN MFUMO WA MAKOMBORA

Pretoria, Afrika Kusini


MTANDAO wa habari wa mybroadband umeripoti kuwa Afrika Kusini inakusudia kuiuzia Iran mfumo wa makombora ya ardhini hadi angani.

Ripoti hiyo iliyonukuliwa na Shirika la Habari la Tasnim inasema, Afrika Kusini imelitaarifu Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu mpango wake huo wa kuiuzia Iran mfumo wa makombora wa Umkhonto kwa gharama ya Dola za Marekani milioni 118.

Mfumo wa makombora ya ardhini hadi angani-Umkhonto umekuwa ukitumiwa na kikosi cha majini cha Meko A200 class cha Afrika Kusini tangu mwaka 2001 na unahesabiwa kuwa moja ya mifumo ya makombora yenye uwezo mkubwa katika kulenga shabaha.

Mwaka jana, Iran na Afrika Kusini zilitia saini hati ya maelewano ya ushirikiano wa kiulinzi na kijeshi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles