27.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 18, 2024

Contact us: [email protected]

Afrika itafakari mdororo biashara ya mafuta na gesi

Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (kushoto) akizungumza na Balozi wa Finland nchini Bi. Sinikka Antila na wajumbe wake walipo tembelea wizara.
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (kushoto) akizungumza na Balozi wa Finland nchini Bi. Sinikka Antila na wajumbe wake walipo tembelea wizara.

Na Joseph Lino,

Mdororo na kushuka kwa bei ya mafuta ulimwenguni kumesababisha kupungua kwa shughuli za sekta hiyo barani Afrika na kuleta jakamoyo  na changamoto  za kiuchumi kwa baadhi ya nchi zinazotegemea  kwa kiasi kikubwa  mapato yao kutoka mafuta na gesi.

Hata hivyo, Afrika bado inatoa fursa nyingi za sekta hii, kwa maelezo ya Mshauri wa mafuta na gesi kutoka kampuni ya ukaguzi wa mahesabu, Pricewatercoopers (PwC), Chris Bredenhann.  Ambaye anasema kwa msisitizo kuwa :

“Ni wakati wa fursa kwa serikali za Afrika ambao wanataka kuvutia wawekezaji wa mafuta na gesi kuboresha mifumo ya udhibiti, uchumi na vigezo vya leseni,”.

Anafafanua kuwa, “Ni muhimu sana sekta hii kuangalia changamoto zaidi zinazosababisha kushuka kwa bei na kuzingatia mambo muhimu kwenye sekta na uendelezaji wake.

Katika ripoti ya Africa Oil & Gas Review, 2016’ iliyotolewa na  PwC inasema kuwa kupunguza gharama kwenye sekta kunahitaji ubunifu wa teknolojia ambao utaongezeka.

Ripoti hii inaelezea kuwa huu utakuwa muda mwafaka wa kuanzisha mafunzo ya kuongeza ujuzi, na ubora wa viwango vya makampuni ili kuwapa nafasi wazawa kuingia kwenye sekta kipindi itakapoinuka. Wahenga walisema mwenzio akinyolewa wewe tia maji.

Wachambuzi wa ripoti wanaelezea  kutoridhika na kipindi cha miezi 12 iliyopita katika soko la mafuta na gesi.

Mwishoni mwa 2015, Afrika imethitisha hifadhi ya gesi yenye futi za ujazo trilioni 496.7 (Tcf), hata hivyo asilimia 90 ya gesi inayozalishwa  Afrika inatoka Nigeria, Libya, Algeria na Misri. Afrika ya Mashariki ni kwanza alfajiri.

Njia za kupambana na  mdororo  wa bei

Changamoto kubwa zilizotambulika na taasisi za sekta ya mafuta na gesi bado hazijabadilika kama mfumo wa udhibiti, rushwa, miundombinu na kukosekana kwa ujuzi.

Na mwaka huu changamoto kubwa kwenye sekta imekuwa kufikia kiwango cha kodi kinachotakiwa na pia mahusiano ya makampuni ya mafuta na gesi na serikali.

Pia wadhitibi kwenye sekta hii bado wameendelea kuwa changamoto kubwa katika biashara ya mafuta na gesi kwa miaka mitatu mfululizo, ikiwa asilimia 70 ya makampuni yametaja kuwa moja miongoni mwa changamoto tano kubwa.

Kwa mara ya kwanza mfululizo wa ripoti za PwC tangu 2010 kuna changamoto sita kubwa Afrika ambazo makampuni ya mafuta  yamekuwa yakikumbwa nazo hasa katika kupata miradi mipya.

Hii inathibitisha huwa ni vingumu sana kwa nchi ambazo hifadhi za mafuta zimegundulika kama Msumbiji kwa sababu serikali inakuwa bado hazielewi taarifa za miradi ya gesi na mafuta.

Kwa sababu hiyo makumpuni mengi wameanza kuwa rafiki na kushirikiana na serikali hizo ili kuhakikisha kuwa kuna mipango.

Makampuni wametambua bei za gesi na mafuta kama  kigezo kikubwa chakuathiri biashara zao miaka mitatu ijayo.

Makampuni hayo yanategemea bei kupanda na kufikia dola za Marekani 52 mwishoni mwa mwaka huu, na dola 60 kufikia mwishoni mwaka 2017 na ifikapo 2018 bei itakuwa dola 69.

Kutokana na udhibiti wa bei kuwa mdogo, biashara zinaelekeza nguvu katika ufanisi na ubora ambao unaweza  kushusha bei ya mafuta.

Changamoto ya pili ni mamlaka za udhibiti bado ni tatizo kwa makampuni mwaka huu kwa kukosa imani ya dhamira na matendo.

Mabadiliko ya thamani ya ubadilishaji wa fedha za kigeni usiotabirika nayo ni changamoto ya tatu ambayo inaweza kuathiri biashara hii miaka mitatu ijayo kwa kukosa mwelekeo.

Fedha na uwekezaji

Kumekuwa  na mazingira ya kurejea kwa bei ya mafuta, bado imani ya wawekezaji imekuwa ndogo kwa sababu kurejea kwa bei bado hakujatulia na soko la mafuta bado lipo chini na Marekani kuendelea kuyumbisha soko kwa kuongeza mafuta na kupunguza matumizi yake .

Bei ya chini ya mafuta imesababisha kwa ujumla wake makampuni kutofikia maamuzi ya mwisho ya uwekezaji miradi ya dola za kimarekani bilioni 300.

Miradi endelevu
Kwa hali ya uchumi iliyopo sasa makampuni ya mafuta na gesi yanatafuta sehemu muhimu za kuwekeza ili kuongeza nguvu katika ukuaji wa biashara ya mafuta miaka mitatu ijayo.

“Sekta ya mafuta na gesi inakumbana  na changamoto za tekinolojia na ajira ambazo hutumia gharama kubwa sana,” anafafanua Bredenhann.

Aidha anasema uendelevu wa sekta hii utaathiriwa na baadhi ya mambo kama bei ya mafuta, nishati mbadala, washidani wapya, athari za mazingira, mifumo na sheria za udhibiti, miundombinu ya tekinolojia ambayo ni nguzo muhimu katika sekta hii.

Asilimia 20 ya makampuni wanamini kuwa miundombinu itakuwa na mchango mkubwa katika biashara zao miaka mitatu ijayo, hata hivyo asilimia 20 wanatarajia tekinolojia kuwa na mchango mkubwa miaka mitatu ijayo.

Mifumo ya udhibiti na miongozo

Mifumo ya udhibiti na miongozo katika sekta ya mafuta na gesi limekuwa jambo kubwa kushughulika nalo.

Tangu 2015,  Afrika Kusini kumekuwepo mijadala ya serikali kutenganisha sheria na sera za mafuta na gesi na sekta ya madini.

Aidha, Mamlaka ya Minerals and Petroleum Resources Development Act (MPRDA) bado ya haijathibitisha au kupitisha hilo.

Kwa upande wa Tanzania, mamlaka ya udhibiti bado haijaeleweka baada ya maboresho sheria ya mafuta  ya 2015, na nchini Nigeria, serikali imeshindwa kupitishwa mswada wa mafuta kuwa sheria.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles