25.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Africa yamlilia Mkapa

Mwandishi wetu

RAIS Uhuru Kenyatta wa Kenya, ametangaza siku tatu za maombolezo ya kitaifa kutokana na kifo cha Benjamin Mkapa.

Kenyatta pia ametangaza bendera ya Kenya na ile ya Afrika Mashariki liwa zitapepea nusu mlingoti nchini humo na kwenye balozi zake zote kuanzia Julai 27 hadi 29 kuomboleza kifo hicho.

 “Katika kumkumbuka Mkapa na katika na kuonyesha mshikamano wa taifa na watu wa Tanzania, bendera ya Kenya na bendera ya Jumuiya ya Afrika Mashariki katika majengo ya umma, viwanja vya umma na kwenye balozi zote za Kenya nje zitapepea nusu mlingoti,” alisema Kenyatta.

Raila Odinga

Mwanasiasa wa upinzani nchini Kenya, Raila Odinga, kupitia ukurasa wake wa Twitter aliandika kuwa Mkapa alikuwa rafiki wa Kenya na watu wa Kenya. 

Alisema wataendelea kumkumbuka jinsi alivyokuwa msuluhishi wa mgogoro wa uchaguzi wa Kenya mwaka 2007-2008 akishirikiana na DK Koffi Annan na Graca Machel, wakati nchi hiyo ilipotumbukia kwenye machafuko kutokana na matokeo ya uchaguzi ambapo kambi ya Odinga ilidai kuibia kura.

“Mkapa alikuwa muunini wa ushirikiano wa kikanda, alichochea kufufuliwa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Afrika imepoteza mtu mkubwa,” alisema.

Kagame

Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Rais wa Rwanda, Paul Kagame alituma salamu za rambirambi kwa Rais John Magufuli na familia ya Mkapa kutokana na kifo hicho.

Alisema kifo cha Mkapa ni pigo kwa Afrika kwani alikuwa muumini wa kweli wa Pan Africa ambaye mchango wake ulikuwa hadi nje ya mipaka ya Tanzania.

Ramaphosa

Kwa upande wake Rais wa Afrika Kusuni, Cyril Ramaphosa kupitia ukurasa wa twitter wa Ikulu ya nchi hiyo, alituma salamu za rambirambi kwa Watanzania kwa kifo cha Mkapa.

Naye Rais wa Zimbabwe, Emmerson Mnangagwa, alituma salamu za rambirambi kwa Rais Magufuli akisema uridhi aliocha utaishi milele.

Bobi Wine

Naye Mwanasiasa kijana wa Uganda, Bobi Wine, alimlilia Mkapa akisema atakumbukwa kwa alivyokuwa muumini wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

“Rais Benjamin Mkapa alitumikia taifa lake kwa bidii na alistaafu kwa amani. Alithamini demokrasia, tunamsaluti kwa mchango wake wa kufufua jumuiya ya Afrika Mashariki. Pumzika vizuri,” alisema Boni Wine.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles