27.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

AFISA MTENDAJI KATA KIZIMBANI KWA KUJERUHI

ERICK MUGISHA – DAR ES SALAAM

AFISA MTENDAJI WA KATA Syridion Michael (40) mkazi wa kinondoni amepandishwa kizimbani katika mahakama ya hakimu mkazi kinondoni kwa kosa la kujeruhi.

Akisomewa hati ya mashtaka mbele ya hakimu Happiness Kikoga na Wakili wa Serikali Ester chale alidai Agosti 1, 2019 eneo la kinondoni mkwajuni wilayani kinondoni Dar es salaam alimng’ata upande wa kulia wa mdomo mtu mmoja Tanya Tasaluko na kumsababishia maumivu.

Mshtakiwa alikana kutenda shtaka hili na wakili wa serikali alidai upelelezi wa shauri hili hauja kamilika aliomba tarehe nyingine kwa kutajwa na kwa kukamilisha upepelezi.

Hakimu Kikoga alisema dhamana kwa mshtakiwa ipo wazi kwa masharti ya kuwa na wadhamini wawili waaminifu, barua za utambulisho, nakala ya vitambulisho vya taifa na kusaini bondi ya sh 500,000.

Hata hivyo mshtakiwa alirudishwa rumande kwa kushindwa kutimiza masharti ya dhamana na kesi yake itakuja kwa kutajwa tena octoba 15 mwaka huu.

Wakati huo huo MKAZI  wa kigogo Ashirafu Abdul (19) amepandishwa kizimbani katika mahakama ya hakimu mkazi kinondoni kwa kosa la kumiliki majani aina ya Bangi gram 66.85.

Akisomewa hati ya mashtaka mbele ya hakimu Happiness kikoga na Wakili wa serikali Ester chale alidai Agosti 7, 2019 eneo la kigogo mbuyuni wilayani kinondoni Dar es salaam alikutwa akimiliki majani yaliyo katazwa kinyume na sheria aina ya bangi gram 66.85.

Mshtakiwa alikana kutenda shtaka hili mbele ya mahakama na wakili wa serikali Ester alidai upelelezi wa shauri hili hauja kamilika aliomba tarehe nyingine kwa kutajwa.

Hakimu kikoga alisema dhamana kwa mshtakiwa ipo wazi kwa masharti ya kuwa na wadhamini wawili waaminifu, barua za utambulisho,nakala ya vitambulisho vya taifa na kusaini bondi ya sh 1,000,000.

Mshtakiwa yupo nje kwa dhamana kwa kutimiza masharti ya dhamana na kesi yake itakuja kwa kutajwa tena octoba 16 mwaka huu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles