28.4 C
Dar es Salaam
Sunday, November 28, 2021

Afariki ajalini akiiba pikipiki

Gurian Adolf – Sumbawanga

MKAZI wa Kijiji cha Ninga, Wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa, Steven Kalunga (29), amefariki dunia katika Kijiji cha Miangalua wilayani Sumbawanga wakati akiwa katika jaribio la kuiba pikipiki na fedha.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, Jastin Masejo, alisema kuwa tukio hilo lilitokea Machi 17, saa 2 usiku katika kijiji hicho.

Kamanda Masejo alisema kuwa siku ya tukio hilo Kalunga akiwa na mwenzake ambaye jina lake halikufahamika mara moja, walitega waya mgumu barabarani ambapo mwendesha pikipiki aliyefahamika kwa jina la Joseph Kachingwe alipata ajali na kuanguka kutokana na mtego huo.

Baada ya mwendesha pikipiki huyo kuanguka na kuumia, ndipo Kalunga na mwenzake huyo waliweza kumvamia na kumpora fedha kiasi cha Sh milioni 1.5 pamoja na pikipiki yake yenye namba za usajili MC 617 CCG na kuipanda kisha kukimbia nayo.

Kachingwe alifanikiwa kuinuka na kupiga kelele za kuomba msaada ndipo kundi la watu walipojitokeza kwa lengo la kumsaidia na walianza kuwafukuza watuhumiwa na kutokana na kuwa na mwendo kasi mkubwa walipata ajali na kuanguka.

“Katika ajali hiyo, Kalunga aliumia vibaya ndipo walipomkamata na kumkimbiza Kituo cha Afya Laela, lakini alifariki dunia wakati akiendelea kutibiwa, huku mtuhumiwa mwingine alifanikiwa kukimbia na fedha ambazo walizipora,” alisema Kamanda Masajo.

Alisema kuwa juhudi za kumtafuta mtuhumiwa aliyekimbia bado zinaendelea ili afikishwe mahakamani kwa mujibu wa sheria.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,206FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles