30.2 C
Dar es Salaam
Sunday, September 25, 2022

AFANDE SELE AIKUBALI NDOA YA ROMA

NA SHARIFA MMASI-DAR ES SALAAM


MKALI wa hip hop nchini, Seleman Msindi ‘Afande Sele’, amesema anavutiwa na ndoa ya msanii mwenzake, Ibrahim Mussa ‘Roma Mkatoliki’, kwani inamkumbusha furaha aliyowahi kuwa nayo kipindi cha uhai wa mke wake, Asha Mohammed.

Afande Sele anayeendelea kutamba na wimbo wa ‘Miaka Kumi’, alisema maisha ya Roma ni darasa tosha kwa wanandoa wachanga, akiwamo rafiki na mdogo wao, Stamina.

“Roma na mke wake ni miongoni mwa wanandoa ninaowakubali kutokana na namna walivyoamua kuishi.

“Wawili hawa wana kila sababu ya kuigwa, binafsi nilipokuwa na mwenzangu mama Tunda, nilikuwa na furaha sana ndio maana hadi sasa naendelea kubaki kama nilivyo kwa kuwa ndoa haihitaji kukurupuka,” alisema Afande Sele.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
201,896FollowersFollow
553,000SubscribersSubscribe

Latest Articles