24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

ADHABU ZA WATOTO ZISITOLEWE ADHARANI

mwanafunzi-akichapwa

HATUA za makuzi anazozipitia  mtoto  ni wazi kuwa yapo makosa ambayo anayafanya na kuhitaji kukanywa kama motto, pia vipo vitu ambavyo anapaswa aelekezwe.

Mtoto anapokosea mzazi  unapaswa  kutumia njia sahihi  ya kumelewesha na si kumuongelea  maneno machafu ama kumkanya mbele za watu, si sawa  na huwezi kumsaidia.

Mara nyingi wazazi wanawaadhibu watoto mbele ya wenzao, jambo hilo siyo zuri pia, linaweza likaonekana kama sehemu ya udhalilishaji.

Unapofanya hivyo kama mzazi unapaswa kutambua kuwa mtoto anakosa ujasiri mbele ya wenzake.

Unapomsema mtoto mbele za watu ni wazi  kuwa anajisikia vibaya, kwakuwa pamoja na yeye kuwa na umri mdogo, lakini bado ni binadamu, hivyo anahitaji kuelekezwa kwa utaratibu.

Kuwaaibisha watoto mbele ya wengine si sawa, hata kama mtoto ni mdogo ni vyema kumchukua  na kumpeleka mahali pa faragha na kumweleza kosa.

Kabla ya kumuadhibu unapaswa kumpa nafasi ya kujitetea na endapo utagundua amekosea unapaswa kumuadhibu, si mbele za watu.

Wazazi lazima tukumbuke kuwa watoto nao ni watu kamili walio na hisia, utashi, aibu nk, ni muhimu kuwaheshimu.

Mbali na hilo, adhabu kali kupita kiasi, wazazi ni lazima wapime adhabu wanazotoa kwa watoto wao kulingana na kosa, jinsia, umri na mazingira pia.

Vilevile adhabu isitolewe kwa hasira, vinginevyo mtoto hataelewa kosa na anaweza akarudia kama hakuelewa.

Wapo ambao hawapendi kuwapa adhabu watoto wao, hivyo anaamua kumkemea bila kuchukua hatua yoyote, mara nyingi utasikia kwa mama au baba akimwambia mtoto, kwa mfano, “acha!, nitakupiga wewe.” Mtoto anaendelea tu kufanya anachofanya na mzazi wala hamchapi.

Hali hii inamjengea mtoto kuona kuwa mzazi ana tabia ya kusema au kufoka tu, bila kuchukua hatua yoyote.

Kufanya hivyo ni mbaya sana kwa motto, kwanza unamtengenezea mazingira ya kuwa na kiburi, kutokuwa msikivu wala mtiifu kwa watu waliomzidi.

Ni vizuri mzazi akimwambia mtoto “acha” au “njoo” au “nenda” na mtoto asipotii kufanya, unatakiwa umsaidie  kutekeleza aliloambiwa ili aumbike tabia ya kutii.

Jenga utaratibu mzuri wa kuongea na mtoto uweze kumjenga kuwa mtu mwenye tabia  nzuri na heshima kwa wakubwa na watoto.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles